Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kununua vifaa tiba – Dkt. Dugange
HomeHabari

Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kununua vifaa tiba – Dkt. Dugange

Na Fred Kibano, D’Salaam Serikali imetumia jumla ya shilingi Bilioni 95.37 ambazo zimetumika kununua vifaa tiba na kupelekwa kwenye vitu...


Na Fred Kibano, D’Salaam
Serikali imetumia jumla ya shilingi Bilioni 95.37 ambazo zimetumika kununua vifaa tiba na kupelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya ili kuboresha afya za wananchi na ustawi wa Taifa.

Kauli hiyo imetolewa na Dkt.Festo Dugange, Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) jana Jijini Dar es Salaam wakati akitoa maelezo ya awali kwenye Mkutano wa 22 wa Mapitio ya Sera na mafanikio kwenye Sekta ya Afya ambao unafanyika kila mwaka.

“Serikali imeweza kununua Vifaa Tiba vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 95.37 kupitia fedha ya mkopo nafuu kutoka Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kwa ajili ya Vituo vya kutolea huduma za Afya katika ngazi ya Halmashauri” alisisitiza Dkt. Dugange.

Dkt. Dugange amesema pia Halmashauri zinaendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya majengo ya Idara ya dharura (EMD) - 80, Wagonjwa mahututi (ICU) - 26, Nyumba za Watumishi 150 katika Vituo vya kutolea huduma za Afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 44.5 kupitia fedha za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ambayo ni mapinduzi makubwa katika Sekta ya Afya.

Aidha, kuhusu ujenzi wa vituo vya afya amesema hadi kufikia mwezi Novemba, 2021 Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilipeleka fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 55.25 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya 221 katika maeneo ya kimkakati kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini.

Akifungua Mkutano wa 22 wa Mapitio ya Sera na mafanikio kwenye Sekta ya Afya Dkt. Dorothy Gwajima amesema, Serikali katika ngazi ya Msingi imefanikisha kusajili zahanati 5,325, vituo vya afya 629 pamoja na Hospitali za Wilaya 68 ambazo zote zinatoa huduma. Aidha, vituo vipatavyo 415 vinatoa huduma ya dharura ya upasuaji kwa mama wajawazito na huduma kwa Watoto wachanga hali iliyoongeza mwamko kwa kina mama kuhudhuria kwenye vituo vya afya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifello Sichalwe, amesema Serikali inaendelea kuimarishaji mifumo ya TEHAMA ikiwa ni pamoja na mfum Afya-Care na GoTHOMIS ambayo itasaidia kuimarisha takwimu za afya na mipango ya afya inayopimika kwa kuweka vipaumbele vinavyolingana na takwimu kupitia mifumo hiyo.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kununua vifaa tiba – Dkt. Dugange
Serikali imetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 95 kununua vifaa tiba – Dkt. Dugange
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgmH1a5EaAJ6ChPdhdmjfX8vsSNEDQH7x2LA67RGm9JgDu3V07ukgV4Bud5geIdVndxBodFZAP52TmwBezMp-QGEx15oHulQKjkEEt7oamEvvATGr8_AfHxLwW3jhqD8IB_lDhJfik58SylrDsTOOQjut6KsT-dlkRJpdIjjdLGVOzQE6v7AhBjKPg9aQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgmH1a5EaAJ6ChPdhdmjfX8vsSNEDQH7x2LA67RGm9JgDu3V07ukgV4Bud5geIdVndxBodFZAP52TmwBezMp-QGEx15oHulQKjkEEt7oamEvvATGr8_AfHxLwW3jhqD8IB_lDhJfik58SylrDsTOOQjut6KsT-dlkRJpdIjjdLGVOzQE6v7AhBjKPg9aQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/serikali-imetumia-zaidi-ya-shilingi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/11/serikali-imetumia-zaidi-ya-shilingi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy