Bashungwa awajulia hali majeruhi ajali Biharamulo,abiria 11 wapoteza maisha
HomeHabariTop Stories

Bashungwa awajulia hali majeruhi ajali Biharamulo,abiria 11 wapoteza maisha

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amefika eneo ilipotokea ajali ya basi la abiria lenye namba za usajili T857 DHW, katika...

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amefika eneo ilipotokea ajali ya basi la abiria lenye namba za usajili T857 DHW, katika eneo la Kabukome katika Kata ya Nyarubango wilayani Biharamulo mkoani Kagera na kuwajulia hali majeruhi wanaoendelea kupewa matibabu katika hospitali teule ya biharamulo, tarehe 21 Disemba 2024.

Basi hilo liliokuwa linafanya safari kutoka Kigoma kwenda Bukoba wakati liliposimama kushusha abiria ambae alipitilizwa kwenye kituo, lilishindwa kuondoka na kuanza kurudi nyuma kisha kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo imesababisha vifo vya abiria 11 na majeruhi 16 ambapo Majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospitali teule ya Biharamulo mkoani Kagera.

Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi, Waziri Bashungwa ametoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wote walioguswa na ajali hiyo na kutoa wito kwa Watanzania kuendelea kuwaombea majeruhi wapone haraka.

“Nitumie nafasi hii kuombea raho za marehemu ambao tumewapoteza katika ajali ambayo imetokea hapa Biharamulo, tumepoteza ndugu zetu 11, wametangulia mbele za haki” amesema Bashungwa

Aidha, Bashungwa ameeleza kuwa Wizara imeanza kufanyia kazi Maelekezo ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufanya marekebisho ya kuwa na mfumo wa leseni za udereva ili kuwapunguzia alama madereva wanafanya makosa yenye kuhatarisha usalama barabarani ambazo zitapelekea kuwafungia leseni.

Kwa Upande wake, Mganga mkuu wa Hospitali teule ya Biharamulo, Gresmus Sebuyoya ameeleza kwa majeruhi 26 wameruhusiwa na wengine 16 wanaendelea na matibabu na ungalizi wa karibu.

“tumebaki na watoto wanne ambao wanaendelea vizuri, wanaume tunao sita, vifo tulikuwa navyo kumi na moja, wanawake watano, wanaume wanne na watoto wawili” ameeleza Daktali Gresmus.

 

The post Bashungwa awajulia hali majeruhi ajali Biharamulo,abiria 11 wapoteza maisha first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/JhmtI4d
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Bashungwa awajulia hali majeruhi ajali Biharamulo,abiria 11 wapoteza maisha
Bashungwa awajulia hali majeruhi ajali Biharamulo,abiria 11 wapoteza maisha
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241222-WA0019-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/bashungwa-awajulia-hali-majeruhi-ajali.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/bashungwa-awajulia-hali-majeruhi-ajali.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy