Kamati tatu za Bunge zamgomea Makinda
Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kinachojumuisha wenyeviti wote wa Kamati za Bunge kilichokutana jana kupanga ratiba ya mkutano wa Bunge unaotarajiwa kuanza vikao vyake Jumanne ijayo. Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam. Picha na Owen Mwandubya.
HomeHabariKitaifa

Kamati tatu za Bunge zamgomea Makinda

Spika wa Bunge, Anne Makinda (kulia) akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kinachojumuisha wenyeviti wote wa Kamati za Bunge kilichokut...

WAUMINI: MAPADRI WARUHUSIWE KUOA
ANGALIA MAJINA Yote YA WANAFUNZI KIDATO CHA 6 WALIOCHAGULIWA ,JKT KWA MUJIBU 2015 Kupitia simu yako ya Mkononi
MIGOMO YA WANAFUNZI VYUO VIKUU YASAMBAA


Dar es Salaam. Danadana zimeendelea juu ya utekelezaji wa azimio la tatu la Bunge kuhusu kashfa ya Akaunti ya Tegeta Escrow linaloagiza kuwajibika kwa wenyeviti wa kamati zake tatu za kudumu, baada ya juzi Spika wa Bunge, Anne Makinda kukaririwa akisema wameshajiuzulu, lakini wajumbe wake wameibuka jana na kusema hawatafanya uchaguzi hadi watakapopata maelekezo kutoka Ofisi ya Spika.


Azimio hilo ambalo ni moja ya manane ya Bunge hilo linasema: “Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa 18 wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa kamati husika za kudumu za Bunge.”


Wenyeviti hao na kamati zao katika mabano ni Victor Mwabalaswa (Nishati na Madini), Andrew Chenge (Bajeti) na William Ngeleja (Katiba, Sheria na Utawala).


Juzi, Spika Makinda aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wenyeviti waliotakiwa kuvuliwa nyadhifa zao tayari wamejiuzulu na kamati husika zinatakiwa kufanya uchaguzi kupata wengine wapya.


Hata hivyo, jana, kwa nyakati tofauti Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Jerome Bwanausi na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, Dk Festus Limbu walisema hawatafanya uchaguzi mpaka pale watakapopata maelekezo kutoka Ofisi ya Spika, huku wajumbe wa kamati ya Katiba wakieleza hivyohivyo.


Dk Limbu alisema: “Unajua Chenge aliteuliwa na Spika Makinda kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti. Tunachokisubiri ni ruhusa ya Spika ili tufanye uchaguzi, kama anateua tena mwenyekiti basi tunasubiri uteuzi wake.”


Hata hivyo akizungumzia suala hilo la Chenge, Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah alisema: “Chenge aliteuliwa katika kipindi cha mpito ambacho kikiisha atachaguliwa mwenyekiti mwingine. Hivyo alisema naye anaweza kuondolewa tu na wajumbe wa kamati.”


Kwa upande wake, Bwanausi alisema: “Hatuwezi kufanya uchaguzi bila kupata maelekezo kutoka Ofisi ya Spika. Tulichoamua kamati ni kumwondoa Mwabalaswa katika nafasi yake ya uenyekiti, ila kama ni uchaguzi bado hatujafanya.”


Jana, kikao cha Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala kiliongozwa na Nyambari Nyangwine badala ya Ngeleja aliyekiongoza juzi, licha ya kutotakiwa kufanya hivyo kulingana na maazimio ya Bunge.


Wajumbe wa kamati hiyo waliozungumza walieleza kuwa Nyangwine aliongoza badala ya Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Gosbert Blandes ambaye alikwenda kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uongozi.


Dk Kashilillah alisema jana kwamba tayari Spika ameshatoa maelekezo na kinachotakiwa kufuatwa na kamati hizo ni utekelezaji tu. “Kauli ya Spika kwamba wenyeviti wamejiuzulu na kuzitaka kamati husika kufanya uchaguzi tayari ni maelekezo. Sasa hapo unataka tuseme kitu gani, labda andikeni kuwa kamati zimekaidi agizo hilo,” alisema Kashilillah
 
Chanzo MWANANCHI
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Kamati tatu za Bunge zamgomea Makinda
Kamati tatu za Bunge zamgomea Makinda
http://www.mwananchi.co.tz/image/view/-/2599602/highRes/928363/-/maxw/600/-/bwg1j4/-/makinda_kamati.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/kamati-tatu-za-bunge-zamgomea-makinda.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/kamati-tatu-za-bunge-zamgomea-makinda.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy