Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimefanya mashambulizi kwa makombora ya masafa marefu leo yaliyoharibu shehena kubwa ya si...
Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema vikosi vyake vimefanya mashambulizi kwa makombora ya masafa marefu leo yaliyoharibu shehena kubwa ya silaha kutoka mataifa ya magharibi katika eneo la kusini mashariki mwa Ukraine.
Taarifa ya wizara hiyo imearifu kwamba shambulizi kwenye kiwanda cha alumini katika jimbo la Zaporizhzhia (Zapori'ja) limeteketeza hifadhi kubwa ya silaha na risasi zilizotolewa na Marekani na mataifa ya Ulaya kulisaidia jeshi la Ukraine.
Hayo yanajiri siku moja baada ya Marekani na mataifa mengine 40 kufanya mkutano wa usalama nchini Ujerumani kujadili kuipatia silaha zaidi Ukraine huku Washington ikiapa kulisaidia taifa hilo kushinda vita kati yake na Urusi.
Ingawa Urusi hakusema aina ya silaha zilizoharibiwa katika shambulizi la leo, inafahamika kuwa Ukraine imekuwa ikipokea risasi, makombora na mizinga ya kudungua ndege kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS