Serikali Kuboresha Upatikanaji Wa Huduma Za Dawa Nchini
HomeHabari

Serikali Kuboresha Upatikanaji Wa Huduma Za Dawa Nchini

 Na WAF – Dodoma Serikali kupitia Wizara ya afya imejipanga kukabiliana na ukosefu wa dawa muhimu katika vituo mbalimbali vya kutolea hu...

6 ICT Job Opportunities at the Tanzania Posts Corporation (TPC)
Visa yakwamisha safari ya Miss Tanzania kushiriki Miss World 2021
Mvua kubwa kunyesha kuanzia kesho


 Na WAF – Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya afya imejipanga kukabiliana na ukosefu wa dawa muhimu katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.


Hayo yamesemwa  na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii wakati akiwasilisha randama ya bajeti ya Wizara mwaka wa fedha 2022/2023. 


Waziri Ummy amekiri kuwa na uhaba wa dawa katika vituo vingi vya kutolea huduma za afya nchini huku sababu ikitajwa kuwa ni kutozingatia mpango kazi wa manunuzi ya dawa pamoja na matumizi na usimamizi katika ngazi za vituo vya kutolea huduma za afya.


“Maoteo ya dawa yanatakiwa kuletwa Wizarani kutoka katika vituo vya kutolea huduma, tumeshaonesha magonjwa kumi yanayoongoza nchini hivyo inatakiwa kila kituo kijue ni magonjwa gani yanayoongoza kwa wananchi wa eneo hilo. Hivyo kituo kiweke mpango kazi wa manunuzi pamoja na matumizi sahihi ya dawa ili kuepusha kukosekana na kupelekea kero kwa wananchi”. Amesema Waziri Ummy.


Waziri Ummy ameongeza kuwa ni jukumu la Mganga Mkuu wa Wilaya kupitia maoteo yanayoletwa kutoka katika vituo kama ni sahihi yaende ngazi ya mkoa na kisha Wizarani. Hatua hii itasaidia wizara kupanga bajeti ya dawa ambayo itakidhi mahitaji ya nchi.


Kwa upande wake Naibu Waziri wa afya Dkt. Godwin Mollel amesema mfumo wa ununuzi wa dawa katika bohari ya dawa (MSD) bado unaleta changamoto kwenye vituo vya kutolea huduma ambapo dawa zinapoagizwa hazifiki kama mahitaji yanavyotaka. 


Dkt. Mollel amesema hali hii husababisha ukosefu wa dawa katika vituo na kuwafanya watoa huduma kuwaandikia wagonjwa fomu za kwenda kununua katika maduka binafsi.


Ili kutatua changamoto hiyo pamoja na nyingine Waziri Ummy aliiomba kamati ya kudumu ya bunge ya huduma na maendeleo ya jamii kupitisha bajeti ya Shilingi Trilioni 1.109 kwa ajili ya uendeshaji wa Wizara ya Afya ambapo wajumbe wa kamati wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti Mhe. Aloyce Kamamba ilipitisha na kuwa bajeti rasmi ya mwaka 2022/2023.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Kuboresha Upatikanaji Wa Huduma Za Dawa Nchini
Serikali Kuboresha Upatikanaji Wa Huduma Za Dawa Nchini
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhg9aSHnL_oTJzru5VdF-B4BvyyARpqKjEwagOkC5NexNppJdS8qSLQmAmd1YUj3Momw-Swet-DvNpe_wRdHiR3d-a8LFgi6zWRrfz2nZo7qUbaBvKM27uwDIxC2yNk25iFffJfW0g3CJupif7rM3Xl0uZ4EncaKvXJwYNBnSRhCuE72EGD03igXzueFQ/s16000/1.webp
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhg9aSHnL_oTJzru5VdF-B4BvyyARpqKjEwagOkC5NexNppJdS8qSLQmAmd1YUj3Momw-Swet-DvNpe_wRdHiR3d-a8LFgi6zWRrfz2nZo7qUbaBvKM27uwDIxC2yNk25iFffJfW0g3CJupif7rM3Xl0uZ4EncaKvXJwYNBnSRhCuE72EGD03igXzueFQ/s72-c/1.webp
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/serikali-kuboresha-upatikanaji-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/03/serikali-kuboresha-upatikanaji-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy