Rais wa Ukraine Volodymir Zelenskiy amelaani hatua ya Urusi kutambua uhuru wa majimbo yanayoshikiliwa na waasi mashariki mwa nchi yake, n...
Rais wa Ukraine Volodymir Zelenskiy amelaani hatua ya Urusi kutambua uhuru wa majimbo yanayoshikiliwa na waasi mashariki mwa nchi yake, na kuongeza kuwa Ukraine haitaruhusu kupokonywa ardhi yake.
Akilihutubia taifa baada ya uamuzi wa Urusi kusainiwa na rais wake, Vladimir Putin, Zelenskiy amesema licha ya hatua hiyo ya Urusi, mipaka ya Ukraine itabaki kama ilivyo.
Wakati huo huo kiongozi huyo wa Ukraine amezitaka nchi za magharibi kuiwekea Urusi vikwazo vikali, akisema huu ni muda ambapo Ukraine itawatambua marafiki wa kweli.
Vile vile amesema nchi yake itaendelea katika njia ya diplomasia kwa sababu inataka amani.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS