KIDUKU ATAJA CHANZO CHA JINA LAKE,YEYE SHOWSHOW
HomeMichezo

KIDUKU ATAJA CHANZO CHA JINA LAKE,YEYE SHOWSHOW

HII hapa simulizi ya Twaha Kiduku ambaye ni bondia wa ngumi nchini Tanzania ambapo amesema kuwa jina hilo lilitokana na mtindo wake wa kun...

SIMBA YAIPOTEZA YANGA, AZAM FC KWENYE REKODI
ARSENAL YAKAMILISHA DILI LA KIUNGO LOKONGA
VIDEO: TANZANIA PRISONS YAPATA DILI NONO, USAJILI WAPIGIWA HESABU

HII hapa simulizi ya Twaha Kiduku ambaye ni bondia wa ngumi nchini Tanzania ambapo amesema kuwa jina hilo lilitokana na mtindo wake wa kunyoa.

Pia ameweka wazi kuwa hakuwa analipenda mwazno ila mwisho likajibu na akaamua kuendelea kulitumia, huyu hapa anasimulia kuhusu maisha yake:


 â€œKikubwa namshukuru Mungu kwa nafasi hii aliyonipa Mungu, nitajitahidi kuitumia vizuri hata kama itakuja kuisha na kuja wengine basi nijue ngumi imenipa nini na nini.

Sasa unampango wowote wa kuanzisha kituo cha vijana kujifunza ngumi?


“ Nilikuwa nao hata kabla sijajulikana maana nilianza kufundisha hata kabla ya kufundishwa maana nilikuwa sijui chochote ila namshukuru Mungu ndiyo nikakutana na mwalimu Pawa Iranda Jeuri ya Tanzania ila GYM ya King Stone bado ipo na mmoja kati ya mabondia wangu walicheza pale.


Jina la Kiduku umelipata vipi?

“Kiukweli jina la Twaha Kiduku lilikuja tu lenyewe kwa sababu mechi yangu ya kwanza nilikuwa nimenyoa Kiduku, sasa wakati wakawa hawajui jina la Twaha wakawa wananiita bondia mwenye Kiduku.

 â€œKiukweli nilikuwa nalichukia sana mwanzoni maana miaka ya nyuma mtu akinyoa Kiduku anaonekana mhuni halafu mimi sina tabia hizo na hata kwenye mechi ya pili sikunyoa Kiduku ila mashabiki wakawa wanashangilia Kiduku…Kiduku.


“Nikaona hili jina limeshakaa na nikawa nikiitwa naitikia hadi nimelizoea na kwa sasa ndiyo limekuwa maarufu zaidi.

Mabondia wengi wamekuwa wakikiri kuwepo kwa mambo ya kishirikina hasa kwa kuwekewa vitu kwenye glavu na wakati mwingine kushindwa kuona, umeshakutana na hali kama hiyo?


“Unajua ninachoamini kila mmoja ana imani yake katika maisha na kama anaiamini imani yake inabidi aifuate.

“Ushirikina upo na kwa sisi wenye imani ya kiislam katika hadithi za dini zinasema mtume wetu alirogwa kwa kuhakikisha kuwa uchawi upo lakini Mungu pia ameshusha uchawi, akashusha na kinga ambazo ni dua.

“Sasa kama unaimani ya ushirikina upo basi kinga yake ni kufanya dua na Mungu anavunja kila kitu, watu hawajui tu kwamba Mungu anampenda mja wake pale anapomlilia shida kwa imani yake thabiti hata usiku wa manane.

“Unajua hata katika pambano lililopita na ndugu yangu yaliendekezwa sana mambo hayo kama uliona watu walipanda na mtu mmoja mlemavu akawa anafanya vitu vya ajabu, siyo vizuri ila ni sehemu ya imani yake.

“Kikubwa ni kwamba namshukuru Mungu, kanipandisha na nimefanikiwa kushinda ila mambo mengine naachana nayo nafaya vitu vingine.

Kuna video moja uliposti mtandao ikimuonyesha huyo ambaye unasema alipanda ulingoni kwenye pambano lako dhidi ya Dullah na ukaandika mganga ni Mungu peke yake yeye akitaka liwe lina kuwa. Kwa nini uliamua kuposti ilikuuma?

“Nimeposti hiyo video kwa sababu moja ili mradi watu wamuamini Mungu, Mungu ndiyo kila kitu na ndiyo muweza wa yote.

“Nilikuwa naamka saa nane za usiku naswali, naenda msikitini, nakutana na watu ambao wamejaliwa elimu kubwa ya dini, nikawa nawaomba waniombee dua ya haki na kweli walikuwa wakiniombea.


Niliwahi kupiga stori na bondia mmoja kwamba hataki mapambano na wewe na hata Crown ambayo wewe umeshinda yeye alikuwa akimpelekea mbwa wake baharini kuoga, hii kwako imekaaje?


“Unajua ninachoamini mimi ni nyodo tu, ushaona, kikubwa sitaki kufocus nayo kwa sababu zile clip nimeziona anataka ajibiwe ila mimi naendelea na mazoezi kwa sababu bondia wa kweli unapomtaka lazima akubali mpigane.

“Muwe kama wa­naume, mnapigana maisha mengine yanaendelea mbele lakini kila siku inakuwa hivyo maana ugomvi wa wadada na wanaume ni tofauti, wadada mmoja anaweza akamshika mwenzie mara eehee sijui hivi na hivi…dela sijui la kuazima…eeh sijui hivi na hivi.

“Mnajibishana mwisho siku hata kushikana hamshikani ila wanaume mmoja anaweza aka­pewa tusi halafu mwingine akam­vaa, sasa mambo hayo yakiende­lea mimi na huo upande wa pili yatakuwa kama ya wadada…jamani mara hivi mara vile sasa mimi sipo hivyo, siwezi kuongea kama mtoto wa kiume ambayo anaya weza, anajua kazi yake ni ngumi basi mnapigana, mnaende­lea.

“Lakini kuwa na magari, magari ndiyo ya kwake kama ana mag­horofa ya kwake, watu hatutaki hayo sisi tuna­chotaka watu waone show hivyo tu, watu wanacho­taka kuona ni ladha.


Ukikutana naye pambano utakuwa tayari kupigana?

“Nitakuwa tayari kupigana kwa sababu watu wanataka kuona ladha na siyo mambo mengine, naomba tuongee mambo mengine hiyo mada tuachane nayo," .


Kutoka Championi



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: KIDUKU ATAJA CHANZO CHA JINA LAKE,YEYE SHOWSHOW
KIDUKU ATAJA CHANZO CHA JINA LAKE,YEYE SHOWSHOW
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNFeyJ2RybSI6InGUYyYzXqWLxRoIGllpEZIynWXUdVxAz7SP2EwHo2ZRAJvA4ImD6REGOW5AkQ76968lGQx78S8fGL-JXRl3sMECuo8m4tEBGmd-uXF4g8xcVa6wIF6yMQKiOTw-1Atuz/w640-h430/KIDUKU.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNFeyJ2RybSI6InGUYyYzXqWLxRoIGllpEZIynWXUdVxAz7SP2EwHo2ZRAJvA4ImD6REGOW5AkQ76968lGQx78S8fGL-JXRl3sMECuo8m4tEBGmd-uXF4g8xcVa6wIF6yMQKiOTw-1Atuz/s72-w640-c-h430/KIDUKU.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/kiduku-ataja-chanzo-cha-jina-lakeyeye.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/kiduku-ataja-chanzo-cha-jina-lakeyeye.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy