Amuua Mama Yake Mzazi Kisha Kumfukia Kwenye Chemba Ya Choo
HomeHabari

Amuua Mama Yake Mzazi Kisha Kumfukia Kwenye Chemba Ya Choo

 Happy Lazaro, Arusha Arusha. Jeshi la polisi Jijini Arusha linamshikilia Patrick Mmasi (24) mkazi wa Njiro, jijini hapa, kwa tuhuma za ...


 Happy Lazaro, Arusha
Arusha. Jeshi la polisi Jijini Arusha linamshikilia Patrick Mmasi (24) mkazi wa Njiro, jijini hapa, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi ,Ruth Mmasi (40)ambaye ni mfanyabiashara maarufu wa madini na kisha mwili wake kuutumbukiza kwenye chemba la choo katika nyumba yake.


Tukio la aina yake limegundulika baada ya raia wema kutoa taarifa za Siri Polisi ambao walikwenda na kubaini mwili huo.


Hata hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha Justine Masejo  akizungumza na waandishi wa habari amesema  taarifa rasmi zitatolewa kesho.


Hata hivyo Masejo amethibitisha polisi kumshikilia  Mmasi kwa tuhuma za kifo cha utata cha  Ruth Mmasi ambaye katika.uhai wake alikuwa mfanyabiashara wa madini.


“Tunamshikilia kijana huyo kwa ajili ya uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo na upelelezi utakapokamilika atafikishwa Mahakamani na taarifa rasmi itatolewa”amesema


Taarifa kutoka kwa ndugu wa marehemu  zinasema tukio hilo liligundulika  juzi baada ya Polisi kufika nyumbani kwa marehemu kufanya upekuzi na kubaini mwili ukiwa ndani ya chemba ya choo.


Kwa mujibu wa ndugu huyo ,mtoto wa marehemu  Patricia Mmasi (19) anayesoma Nchini China, alipata mashaka akiwa china wakati alipojaribu kumpigia simu mama yake Ruth na simu yake kutopatikana kwa muda wote.


Amesema aliamua kusafiri kuja Tanzania kwa sherehe za Xmass na kumuuliza kakaye  Patrick kuhusu kutoonekana kwa mamayake na kutopatikana kwenye simu, ambapo kijana huyo alikuwa akimjibu kuwa kwani mama yako akiondoka huwa ananiaga??? ndipo yeye na ndugu wengine wakaamua kutoa taarifa Polisi.


Aliongeza kuwa Polisi walipofika walifanya upekuzi katika sehemu mbalimbali za nyumba hiyo ya kisasa yenye ghorofa moja na ndipo wakabaini mwili huo ukiwa ndani ya chemba la choo nyuma ya nyumba hiyo na mwili huo umegundulika baada ya siku 14 ukiwa ndani ya chembe hiyo.


Ndugu huyo alidai kuwa marehemu alikuwa akiishi na kijana wake  huyo ambaye ndiye Mtoto wake wa kwanza na mara nyingi walikuwa wakitofautiana .


Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa mwili huo ulikuwa umeanza kuharibika na umehifadhiwa katika hospital ya Mkoa Mount Meru Kwa uchunguzi zaidi.


Kwa Mujibu wa ndugu marehemu Ruth atazikwa nyumbani kwao kesho alasiri katika eneo la Mirerani, Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara.


Wakati huo huo polisi wameonya watu katika kipindi hiki cha siku k kujihusisha na uhalifu kwani Ulinzi umeimarishakatika Maeneo mbalimbali ya Jiji.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Amuua Mama Yake Mzazi Kisha Kumfukia Kwenye Chemba Ya Choo
Amuua Mama Yake Mzazi Kisha Kumfukia Kwenye Chemba Ya Choo
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhy9jZJwlYEWu7rK3JDIVU6mSVP3D_fhOQLQYRbraFBai93z5bG09SwNnVMFc-mMRJTD3soyFDyumaYuETOMJ-oxLhaBh7YTwGGNhwmlLZUFAztnZXiKqio5Ra_6njIbQtw9VJXohAJ_us_IvUXvG2LIwqf4rXUxVn2SCr4cXMWEhujYn8lkhRtHUcpqg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEhy9jZJwlYEWu7rK3JDIVU6mSVP3D_fhOQLQYRbraFBai93z5bG09SwNnVMFc-mMRJTD3soyFDyumaYuETOMJ-oxLhaBh7YTwGGNhwmlLZUFAztnZXiKqio5Ra_6njIbQtw9VJXohAJ_us_IvUXvG2LIwqf4rXUxVn2SCr4cXMWEhujYn8lkhRtHUcpqg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/amuua-mama-yake-mzazi-kisha-kumfukia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/amuua-mama-yake-mzazi-kisha-kumfukia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy