IMEELEZWA kuwa kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya ameongeza dili la miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabosi wake hao. Licha ya ...
IMEELEZWA kuwa kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya ameongeza dili la miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabosi wake hao.
Licha ya kwamba hana nafasi kikosi cha kwanza kwa kuwa namba moja ni Aishi Manula nyota huyo atakuwa hapo mpaka 2023.
Awali nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo kwenda Klabu ya Azam FC ila dili hilo lilibuma.
Kakolanya kwenye mechi za kimataifa msimu huu ambapo Simba iliishia hatua ya robo fainali alicheza mchezo mmoja kwenye hatua ya makundi.
Ilikuwa mbele ya Al Merrikh wakati huo Manula alikuwa anaumwa.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS