R AIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amefunguka kuwa timu za Simba na Yanga ndizo zinampa heshima kubwa katika ...
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallace Karia amefunguka kuwa timu za Simba na Yanga ndizo zinampa heshima kubwa katika mataifa mbalimbali, huku akiwataja mastaa wake bora.
Rais Karia aliyazungumza hayo alipotembelea ofisi za Global Publishers kupitia kipindi maalum ndani ya +255 Global Radio.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Karia alifunguka kuwa baadhi ya mambo ambayo anajivunia ndani ya uongozi wake ni kuwa na uongozi bora ambao umepelekea timu za taifa kufanya vizuri.
Wachezaji anaowakubali
“Wachezaji wetu wa ndani ambao wapo kwenye kiwango bora na ninawakubali ni pamoja na Deus Kaseke, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, John Bocco,Aishi Manula.
"Na kwa wale wa nje ni Luis Miquissone na Haruna Niyonzima. Ila kwa upande wa mchezaji ambaye ni bora na ninampenda sana ni Mzamiru Yassin ambaye amekuwa akipambana kwa ajili ya kupata namba kwenye kikosi.
“Wachezaji wengi wazawa hawajitambui kwani wanashindwa kupambania namba na kuonyesha ubora wao,” alisema Karia.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS