IMERIPOTIWA kuwa kiungo wa Klabu ya Liverpool, Georginio Wijnaldum ameamua kusepa ndani ya Liverpool na anahitaji kujiunga na Klabu ya Ba...
IMERIPOTIWA kuwa kiungo wa Klabu ya Liverpool, Georginio Wijnaldum ameamua kusepa ndani ya Liverpool na anahitaji kujiunga na Klabu ya Barcelona.
Kiungo huyo raia wa Uholanzi anatajwa kukubali mkataba wa awali aliopewa na mabosi wa Barcelona.
Ikiwa usajili wake utakamilika mapema basi utakuwa ni usajili wa kwanza wa Barcelona chini ya Rais mpya Joan Laport ambaye anarudi hapo kwa mara ya pili.
Ndani ya Liverpool ambayo ina kwenda mwendo wa kinyonga ndani ya Ligi Kuu England mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu hivyo atakuwa mchezaji huru.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS