Rais mstaafu Jakaya Kikwete Amlilia Dr Magufuli
HomeHabari

Rais mstaafu Jakaya Kikwete Amlilia Dr Magufuli

  Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ametoa pole kwa Watanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano,...

Juventus watoa pendekezo la £40m kwa Greenwood huku Napoli pia wakionyesha nia.
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 13, 2024
Chelsea wamekubali kumnunua Jhon Duran kwa pauni milioni 42.

 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ametoa pole kwa Watanzania kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Dkt. John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.


Kupitia ukurasa wa Twitter, Dkt Kikwete ameandika ujumbe wa simanzi kufuatia kifo hicho, amesema kumpoteza Dkt. Magufuli ni pigo kubwa lisilomithilika kwani ametutoka ghafla bila ya kutazamia.

“Tungetamani John Pombe Joseph Magufuli tuendelee kuwa nawe leo na miaka mingi ijayo, lakini mapenzi ya Mungu hatuna uwezo kuyabadili. Wajibu wetu ni kumuombea kwa mola ampe mapumziko. Daima tutamkumbuka Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa mema mengi aliyoifanyia nchi yetu. Hakika Tanzania imepoteza kiongozi mzalendo wa dhati, shupavu, mahiri na makini,” imeeleza taarifa hiyo.

Dkt. Kikwete amesema jambo la faraja kwa Watanzania kwa sasa ni kuwepo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye hapo awali alikuwa makamu wake kuanzia mwaka 2015 hadi umauti unamkuta.

Pia ametoa pongezi kwa Samia Suluhu Hassan kwa hotuba yake aliyoitoa baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Nampongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa hotuba fupi na nzuri aliyoitoa baada ya kuapishwa na yenye kujenga imani na kuleta matumaini. Tumuombee Rais wetu kwa Mwenyezi Mungu amuongoze vyema kwa kila uamuzi atakaouchukua na kila hatua atakayopiga.”

Dkt. Kikwete ametoa salam za mkono wa pole na rambirambi kwa Mama Janet Magufuli na familia nzima.
 

 


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais mstaafu Jakaya Kikwete Amlilia Dr Magufuli
Rais mstaafu Jakaya Kikwete Amlilia Dr Magufuli
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhl_loJubK7JpVk-n1aBxc1OcMoW1y6EMlLnvqFjgbNspEp6Sg0HcSnyuc4gxb6Xwwj7-idNKxOlhNhEidTFPzWqv7X3tbITkjcBzxAh79P4ijPgDm7Bh64NmXJ_hITTKv2DGDYoLmRyqwj/s16000/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhl_loJubK7JpVk-n1aBxc1OcMoW1y6EMlLnvqFjgbNspEp6Sg0HcSnyuc4gxb6Xwwj7-idNKxOlhNhEidTFPzWqv7X3tbITkjcBzxAh79P4ijPgDm7Bh64NmXJ_hITTKv2DGDYoLmRyqwj/s72-c/1.png
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-amlilia-dr.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/rais-mstaafu-jakaya-kikwete-amlilia-dr.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy