Dkt Chaula Asisitiza Uwazi Kwa Watendaji Wa Taasisi Za Mawasiliano Zenye Matawi Tanzania Bara Na Visiwani
HomeHabari

Dkt Chaula Asisitiza Uwazi Kwa Watendaji Wa Taasisi Za Mawasiliano Zenye Matawi Tanzania Bara Na Visiwani

Na Faraja Mpina – WMTH, Zanzibar Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula amewataka watendaji wa ...

Mabadiliko: Hayati Dkt. Magufuli Atazikwa Machi 26, 2021....Zanzibar Ataagwa March 23
Njia Utakapopita Mwili wa Dr. John Pombe Magufuli Jijini Dar Es Salaam Asubuhi Hii
Rais mstaafu Jakaya Kikwete Amlilia Dr Magufuli


Na Faraja Mpina – WMTH, Zanzibar

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula amewataka watendaji wa taasisi za mawasiliano zenye matawi Tanzania bara na visiwani kuwa wazi kwa wananchi kwa kutoa maelezo ya kina kuhusu sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ili kuondoa sintofahamu kwa huduma zinazotolewa na taasisi hizo zilizo katika pande zote mbili za muungano ambazo ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) pamoja na Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Hayo ameyazungumza katika kikao cha Makatibu Wakuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (JMT)na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kilichofanyika tarehe 8.3.2021 visiwani Zanzibar.

Dkt. Chaula ameongeza kuwa, taasisi hizo zinatakiwa kuzifahamu, kuzielewa na kuzifanyia kazi sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya utoaji wa huduma wanazozitoa ikiwa ni pamoja na kuelimisha jamii kufuata sheria hizo bila shurti.

“Tulikuwa na hoja nane baada ya kuzichambua zimebaki tano, ambapo kimsingi ni masuala ya kuweka sawa kanuni, taratibu na sheria zetu pamoja na kuongeza uelewa kwasababu lengo kuu la kuzitunga ni kuhakikisha kuwa zinafuatwa”, Dkt.Chaula

Aidha, amesema kuwa kikao kilikuwa kizuri na wataalamu walijipanga vema katika kufanya wasilisho ambapo changamoto mbalimbali zilizowasilishwa zimechukuliwa na kuboreshwa na zitawasilishwa katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo mbili kwa lengo la kuzifahamu na kuzitolea maamuzi ili wananchi waendelee kufurahia muungano.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (SMZ) Amour Bakari amesema kuwa  kikao hicho ni muendelezo wa vikao vya mashirikiano  baina ya taasisi za mawasiliano za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambavyo awali vilianza katika ngazi ya watendaji.

“Kikao cha leo ni cha ngazi ya Makatibu Wakuu, na yale yote yaliyojadiliwa katika kikao hiki yatapelekwa katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizi mbili kitakachofanyika siku ya alhamisi ya tarehe 11.3.2021 hapa Zanzibar”, Amour Bakari

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalin

Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt Chaula Asisitiza Uwazi Kwa Watendaji Wa Taasisi Za Mawasiliano Zenye Matawi Tanzania Bara Na Visiwani
Dkt Chaula Asisitiza Uwazi Kwa Watendaji Wa Taasisi Za Mawasiliano Zenye Matawi Tanzania Bara Na Visiwani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgui7ll19m2b6YXGzDUSWn9c88S1VCyprk2f4R9PWv4whSBBcTpv3MDxBUGE8FkWGFn0REA4dGSBECDBoKnnKPcbX6tu3kFkDpeSR388ZQChGTpnLWtybN-xij9Etd1SJGUb348cTwGFcfV/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgui7ll19m2b6YXGzDUSWn9c88S1VCyprk2f4R9PWv4whSBBcTpv3MDxBUGE8FkWGFn0REA4dGSBECDBoKnnKPcbX6tu3kFkDpeSR388ZQChGTpnLWtybN-xij9Etd1SJGUb348cTwGFcfV/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/dkt-chaula-asisitiza-uwazi-kwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/dkt-chaula-asisitiza-uwazi-kwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy