JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wao wa Merseyside Derby dhi...
JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wao wa Merseyside Derby dhidi ya Everton licha ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0.
Dakika 90 zilikamilika kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England kupiga jumla ya mashuti 15 na sita yalilenga lango huku wapinzani wao Everton wakipiga jumla ya mashuti 9 na sita yalilenga lango.
Mbali na hilo pia umiliki wa mpira kwa Liverpool iliyo nafasi ya 6 na pointi 40 baada ya kucheza mechi 25 ilikuwa ni asilimia 72 huku Everton iliyo nafasi ya 7 na pointi 40 abaada ya kucheza jumla ya mechi 24 ikiwa ni asilimia 28.
Klopp amesema:"Tulicheza vizurri kwenye umiliki pia ilikuwa hivyo hata kushambulia kwetu ilikuwa zaidi yao ila vijana wameshindwa kutumia nafasi, hakuna namna tunajipanga kwa ajili ya wakati ujao,".
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS