Inakadiriwa kuwa watu milioni 12.5 miongoni mwa 32 milioni wanaopatwa na mshituko wa moyo hufariki dunia duniani kote. Mshituko wa m...
Inakadiriwa kuwa watu milioni 12.5 miongoni mwa 32 milioni wanaopatwa na mshituko wa moyo hufariki dunia duniani kote.
Mshituko wa moyo unatokea wakati mtiririko wa damu yenye oksijeni unapozuiwa kwa ghafla katika misuli ya moyo.
Iwapo
mzunguko huo wa damu hautaendelea haraka, kitendo hicho huifanya misuli
ya moyo kuharibika kwa kukosa oksijeni hivyo kuhatarisha maisha ya
muathirika.
Mshituko wa moyo kwa lugha ya tiba unajulikana kama Myocardial Infarction inayomaanisha Myo Muscles au msuli, Cardio… Heart au moyo na Infarct… kufa kwa tishu kutokana na kukosa oksijeni.
Mshituko wa moyo kwa lugha ya tiba unajulikana kama Myocardial Infarction inayomaanisha Myo Muscles au msuli, Cardio… Heart au moyo na Infarct… kufa kwa tishu kutokana na kukosa oksijeni.
Kama
vilivyo viungo vingine mwilini hasa misuli, moyo nao huhitaji damu.
Bila damu seli za moyo hudhoofika mtu kuhisi maumivu. Mshituko wa moyo
Heart Attack kama hutaki kutumia Myocardial Onfarction hutokea pale
mshipa mmoja wa damu au zaidi inaposhindwa kusafirisha damu yenye
oksijeni katika moyo, kutokana na kuziba mishipa hiyo.
Mishipa
ya damu inaweza kuziba kwa sababu tofauti kama vile, kuta za mishipa ya
damu inayopeleka damu kwenye moyo Coronary Arteries kuwa nene,
chembechembe za mafuta kujikusanya katika mishipa ya damu, kudhoofika na
kukonda mishipa ya damu, mishipa ya damu inaposinyaa na kushikana au
kujitokeza donge la damu katika mishipa ya damu.
Mshituko
wa moyo mara nyingi husababishwa na ugonjwa wa moyo wa mishipa ya damu
au Coronary Heart Disease (CHD). Hii ni hali ambayo ndani ya mishipa ya
damu hutokea kitu kiitwacho Plaque na kuzuia damu isiweze kupita katika
mishipa ya damu, ambayo ni matokeo ya muda mrefu.
Lakini
ni wakati gani mtu hukabiliwa na hatari ya kupata mshituko wa moyo? Ni
pale umri wa mtu unapoongezeka na kuwa mzee, mtu anapokuwa na unene wa
kupindukia, kuvuta sigara, kuwa na shinikizo la damu au High Blood
Pressure. Kuishi bila kuwa na harakati na kutoushughulisha mwili. Mtu
kuwa na kiwango cha juu cha mafuta katika damu au High Blood
Cholesterol.
Kuwa na
ugonjwa wa kisukari na kuwa na msongo wa mawazo, wasiwasi na fikra
nyingi. Mambo mengine yanayochangia kupata mshituko wa moyo ni baadhi ya
magonjwa ya moyo, kufanyiwa operesheni ya moyo, kuwa na ndugu katika
familia ambao wana matatizo ya moyo na jinsia ya kiume.
Uvutaji
sigara husababisha mshituko wa moyo unaotokana na kuziba mishipa ya
damu kwa asilimia 36, ambapo unene husababisha ugonjwa huo kwa asilimia
20. Kukaa bila kujishughulisha au kufanya mazoezi husababisha mshituko
wa moyo kwa asilimia 7-12.
Pia
wanaume wanakabiliwa na hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo zaidi
kuliko wanawake katika kipindi chote cha maisha hasa kabla ya wanawake
hawajafikia wakati wa kukatika hedhi. Lakini kwa ujumla kwa kuwa
wanawake huishi miaka mingi kuliko wanaume, magonjwa mengine ya moyo
husababisha vifo vya wanawake uzeeni zaidi kuliko wanaume.
COMMENTS