Kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano, kukojoa kitandani au kujikojolea ni jambo la kawaida. Lakini vijana na watu wazima kujikojo...
Kitabu cha afya ya akili kilichotolewa na Chama cha Madaktari wa Magonjwa ya Akili cha Marekani kinasema kwamba kikojozi ni mtu mwenye tatizo la kujikojolea nguoni au kitandani angalau mara mbili ndani ya kipindi cha wiki moja na kwa muda wa miezi mitatu mfululizo akiwa na umri wa miaka mitano au zaidi. Katika tafiti mbili zilizochapishwa mwaka 2003 kuhusu ukubwa wa tatizo la watoto vikojozi, ilibainika kuwa idadi yao ni kubwa katika jamii kufikia kati ya asilimia 14.7 na 20.
Tafiti kadhaa za afya ya jamii zinabainisha kuwa
watoto wa kiume hukabiliwa zaidi na tatizo hili kuliko wa kike kwa
uwiano wa 2:1.
Pia utafiti mwingine unaonyesha kuwa watoto wa kiume wanakabiliwa na tatizo hili mara tatu zaidi ya watoto wa kike. Katika utafiti uliochapishwa Septemba 2014 katika jarida la kisayansi la IOSR Journal of Dental and Medical Sciences, Dk A.R.C Nwokocha na wenzake wa Chuo Kikuu cha Nigeria walibaini kuwa asilimia 15.82 ya vijana walioko shule za sekondari nchini humo ni vikojozi.
Takwimu nyingine zinaonyesha kwamba katika kila watu wazima 100, mmoja wao ni kikojozi.
Kwa maana hiyo nchi ikiwa na idadi ya watu milioni
50 kama Tanzania, basi idadi ya watu wazima vikojozi inakadiriwa kuwa
ni sawa na nusu milioni.
Ingawa tatizo la kujikojolea linaweza kutokea
wakati wa mchana, ushahidi mwingi unaonyesha kuwa tatizo hili hutokea
mara nyingi zaidi usiku wakati mhusika anapokuwa usingizini.
Hali hii inapomtokea mtoto au mtu mzima, anakuwa hajielewi na ni jambo linalokuwa nje ya uwezo wake katika kujitawala.
Wanasayansi wanatoa sababu nyingi zinazofanya watoto kuwa vikojozi.
Katika utafiti wao Gulnaz Culhal na Nizami Duran wa Chuo Kikuu cha Mustafa Kemal cha nchini Uturuki, walibaini kuwapo kwa uhusiano mkubwa kati ya minyoo aina ya enterobius vermicularis na tatizo la watoto kukojoa kitandani usiku.
Watoto wenye aina hii ya minyoo walikabiliwa na tatizo la kukojoa kitandani kwa asilimia 51.3 na walipotibiwa, tatizo lilipungua hadi kufikia kiasi cha asilimia 28.8.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa katika jarida la European Journal of General Medicine toleo la 3 (1) la mwaka 2006.
Wengine wanahusisha tatizo hili na matatizo ya mishipa ya fahamu kushindwa kumpatia mhusika taarifa ya kujaa kwa kibofu pindi anapokuwa usingizini.
Katika utafiti mwingine uliofanywa na H. Arnell na wenzake na kuchapishwa mwaka 1997 katika jarida la kisayansi lijulikanalo kwa jina la Journal of Medical Genetics, toleo la 34, ilibainika kuwa tatizo hilo lina uhusiano wa karibu na urithi wa vinasaba kutoka kwa wazazi.
Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la Acta Paediatrics toleo la 88.
Wengi hufikiri kuwa watoto vikojozi ni wavivu wa kuamka usiku kwenda kujisaidia au ni watukutu na wanafanya hivyo kwa makusudi. Kutokana na dhana hiyo potofu, wazazi na walezi huwashushia watoto vikojozi kipigo mara kwa mara kama jitihada za kurekebisha tabia za watoto wao.
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni ulioongozwa na Dk Faten Nabeel Al-Zaben wa Kitivo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Mfalme Abdulaziz (King Abdulaziz University) kilichoko Jeddah, Saudi Arabia na kuchapishwa Desemba 2014 na shirika la habari la Reuters, unaonyesha kuwa kuwapa adhabu kali au kuwapiga watoto vikojozi hakusaidii badala yake huongeza ukubwa wa tatizo.
Wazazi wengi hufikiri kuwa wanapowaadhibu watoto kwa kipigo, wataogopa na kuwa makini zaidi wanapolala usiku ili wasikojoe kitandani. Hata hivyo, mara nyingi hushangaa kuona kuwa tatizo linaongezeka na watoto kukabiliwa na fedheha pamoja na msongo mkali wa mawazo ambao huwasababishia hali duni ya afya kwa jumla.
Hyland na wenzake katika utafiti wao uliochapishwa katika jarida la Journal of Behavioral Medicine la Septemba 29, 2012, nao pia walibaini kuwa kipigo cha mara kwa mara kwa watoto kinaweza kusababisha magonjwa sugu kama vile saratani, pumu na magonjwa ya moyo.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa M. Haque pamoja na wenzake uliochapishwa mwaka 1981 katika jarida la Magonjwa ya Watoto la Marekani (Am.J.Dis.Chld) toleo la 135(9).
Mtoto apongezwe mara kwa mara na kupewa zawadi katika siku ambazo hakukojoa kitandani.
Wataalamu wengine wa masuala ya afya na tiba wanasema kwamba
sababu nyingine ni kutokomaa kwa tezi ya pituitary inayopatikana ndani
ya ubongo, chini ya sikio.
Tezi hii ikiwa imekomaa, hutoa homoni inayojulikana kama ADH wakati wa usiku inayopunguza utengenezaji wa mkojo.
Hivyo tezi hiyo inapokuwa dhaifu au kutokukomaa,
husababisha figo kuzalisha kiasi kikubwa cha mkojo na matokeo yake
mhusika akiwa usingizini, hupoteza uwezo wa kudhibiti kiasi kikubwa cha
mkojo kinachozalishwa.
Wengine wanahusisha tatizo hili na matatizo ya mishipa ya fahamu kushindwa kumpatia mhusika taarifa ya kujaa kwa kibofu pindi anapokuwa usingizini.
Sababu nyingine inayotajwa ni uwezo mdogo wa kibofu kushindwa kubeba mkojo wa kutosha kutokana na kulegea kwa valvu zake.
Katika utafiti mwingine uliofanywa na H. Arnell na wenzake na kuchapishwa mwaka 1997 katika jarida la kisayansi lijulikanalo kwa jina la Journal of Medical Genetics, toleo la 34, ilibainika kuwa tatizo hilo lina uhusiano wa karibu na urithi wa vinasaba kutoka kwa wazazi.
Utafiti wa J.N. Bailey na wenzake uliofanyika
mwaka 1999, nao ulibaini kuwepo kwa uhusiano wa karibu kati ya urithi wa
vinasaba na tatizo la watoto kukojoa kitandani kwa asilimia 65 hadi 85.
Utafiti huo ulichapishwa katika jarida la Acta Paediatrics toleo la 88.
Tafiti hizi zote zinabainisha kuwa wazazi vikojozi
au waliokuwa vikojozi zamani wakati wa utoto wao, wana uwezekano wa
kupata watoto vikojozi pia.
Wazazi wengi, walezi na walimu vijana wao hukabiliwa na tatizo la kukojoa kitandani, mara nyingi hawajui chanzo cha tatizo.
Wengi hufikiri kuwa watoto vikojozi ni wavivu wa kuamka usiku kwenda kujisaidia au ni watukutu na wanafanya hivyo kwa makusudi. Kutokana na dhana hiyo potofu, wazazi na walezi huwashushia watoto vikojozi kipigo mara kwa mara kama jitihada za kurekebisha tabia za watoto wao.
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni ulioongozwa na Dk Faten Nabeel Al-Zaben wa Kitivo cha Tiba cha Chuo Kikuu cha Mfalme Abdulaziz (King Abdulaziz University) kilichoko Jeddah, Saudi Arabia na kuchapishwa Desemba 2014 na shirika la habari la Reuters, unaonyesha kuwa kuwapa adhabu kali au kuwapiga watoto vikojozi hakusaidii badala yake huongeza ukubwa wa tatizo.
“Tatizo la watoto kuwa vikojozi huwaathiri wazazi, watoto na
familia kwa jumla. Mara nyingi husababisha aibu na mahangaiko ya kihisia
kwa mtoto mwenye tatizo hilo na watoto wanaoshindwa kupata nafuu
wanaathirika kisaikolojia,” inasema sehemu ya ripoti ya utafiti huo.
Wazazi wengi hufikiri kuwa wanapowaadhibu watoto kwa kipigo, wataogopa na kuwa makini zaidi wanapolala usiku ili wasikojoe kitandani. Hata hivyo, mara nyingi hushangaa kuona kuwa tatizo linaongezeka na watoto kukabiliwa na fedheha pamoja na msongo mkali wa mawazo ambao huwasababishia hali duni ya afya kwa jumla.
Hyland na wenzake katika utafiti wao uliochapishwa katika jarida la Journal of Behavioral Medicine la Septemba 29, 2012, nao pia walibaini kuwa kipigo cha mara kwa mara kwa watoto kinaweza kusababisha magonjwa sugu kama vile saratani, pumu na magonjwa ya moyo.
Utafiti mmoja uliofanyika nchini Marekani kuhusu
wazazi wanaopiga watoto vikojozi ulibaini kuwa, wazazi na walezi wenye
elimu ndogo ndiyo wanaowaadhibu sana watoto wao ambao ni vikojozi kuliko
wale wenye elimu ya kati au wenye elimu ya juu.
Hii ni kwa mujibu wa utafiti wa M. Haque pamoja na wenzake uliochapishwa mwaka 1981 katika jarida la Magonjwa ya Watoto la Marekani (Am.J.Dis.Chld) toleo la 135(9).
Njia bora ya kumsaidia mtoto kikojozi ni kumsaidia
kwa upendo ili aweze kukuza uwezo wake wa kukabiliana na tatizo
linalomkabili.
Mtoto apongezwe mara kwa mara na kupewa zawadi katika siku ambazo hakukojoa kitandani.
Pia ni jambo la busara kumfundisha jinsi ya
kufanya usafi wa nguo zake mwenyewe pale anapojikojolea au anapokojoa
kitandani wakati wa usiku. Wazazi wa watoto vikojozi pia wanashauriwa
kuwapeleka watoto wao kwa madaktari kwa ajili ya kupata tiba stahiki na
ushauri wa kiafya kuliko kutumia njia ya kipigo ambayo ina madhara
makubwa kwa afya ya watoto na inayoongeza ukubwa wa tatizo.
COMMENTS