NCCR-Mageuzi wataka Rugemalira, Tibaijuka, Chenge wafikishwe mahakamani
HomeHabariKitaifa

NCCR-Mageuzi wataka Rugemalira, Tibaijuka, Chenge wafikishwe mahakamani

Dar es Salaam. Chama cha NCCR-Magezi kimesema, vigogo wote waliohusika kutoa na kupokea mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow waf...

Pinda ashukiwa ndani na nje ya Bunge
Rais wa Ujerumani aacha gumzo,aenda Zanzibar kwa boti
KAMATI YA BUNGE YATAKA WALIMU WOTE NCHINI WASAJILIWE

Dar es Salaam. Chama cha NCCR-Magezi kimesema, vigogo wote waliohusika kutoa na kupokea mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Tegeta Escrow wafikishwe mahakamani akiwamo Mkurugenzi wa VIP Engineering Ltd, James Rugemalira .


Kashfa hiyo imesababisha Rais Jakaya Kikwete kufanya mabadiliko madogo ya baraza lake la Mawaziri kutokana na mawaziri wawili kujiuzulu.


Mawaziri waliotajwa kwenye sakata hilo ni Profesa Anna Tibaijuka, ambaye alikuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na aliyeingiziwa Sh1.6 bilioni na mwanahisa wa zamani wa Kampuni ya IPTL, James Rugemarila.


Wengine waliopata mgao huo kutoka kwa Rugemarila na kiasi katika mabano ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge (Sh1.6 bilioni), Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja (Sh40.4 milioni), aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona (Sh40.4 milioni), Mbunge wa zamani wa Sumbawanga (CCM), Paul Kimiti (Sh40.4 milioni) na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Tanesco, Dk Enos Bukuku (Sh161.7 milioni).


Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema waliofikishwa mahakamani hadi sasa ni vidagaa lakini na vigogo mashuhuri wakiendelea kutamba.


“Mpokeaji na mtoaji wa rushwa wote ni wahalifu na wanatakiwa kufikishwa mbele ya mahakama ili wajibu tuhuma zinazowakabili...Rugenarila naye ni miongoni mwa watu wanaotakiwa kufikishwa mahakamani.”


“NCCR tunataka kujua kwa nini baadhi waliopewa rushwa wamefikishwa mahakamani lakini watu wengine kama Profesa Tibaijuka, Chenge, Ngeleja, Yona, Kimiti na wengineo hawafikishwi mahakamani? Wote wanatakiwa kwenda kujibu tuhuma zao,” alisema Nyambabe


Hata hivyo, Mkurugenzi wa Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alipotafutwa kuzungumzia kauli hiyo ya NCCR alisema, “Sipo ofisini hivyo nisingependa kulizungumzia hilo.”


Waliofikishwa mahakamani hadi sasa ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (Rea), Theophillo Bwakea na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma, ambao kwa pamoja wanadaiwa kupokea rushwa ya Sh485.1 milioni.


Wengine ni Meneja Misamaha ya Kodi wa TRA, Kyabukoba Leonard Mutabingwa, Mwanasheria Mwandamizi wa Tanesco, Steven Roman Urassa na Mkurugenzi wa Fedha BoT, Julius Rutta Angello wanaokabiliwa na mashtaka ya kuomba na kupokea rushwa ya jumla ya Sh1.923 bilioni.
 
Chanzo MWANANCHI
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: NCCR-Mageuzi wataka Rugemalira, Tibaijuka, Chenge wafikishwe mahakamani
NCCR-Mageuzi wataka Rugemalira, Tibaijuka, Chenge wafikishwe mahakamani
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSRInSAgAsAbay5YNE2ti9YsmNdAx7uSxelwScEH1xRp7hQaAqgrG2f1tm33AMSRvKWMX4y5NbFlQuCvSOMomNftb8fly9hbRGlmpQtzCjE1BT3jehmNHjGy5mJtCv-HB526NxWiDJ60xX/s640/IMG_3905.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgSRInSAgAsAbay5YNE2ti9YsmNdAx7uSxelwScEH1xRp7hQaAqgrG2f1tm33AMSRvKWMX4y5NbFlQuCvSOMomNftb8fly9hbRGlmpQtzCjE1BT3jehmNHjGy5mJtCv-HB526NxWiDJ60xX/s72-c/IMG_3905.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/nccr-mageuzi-wataka-rugemalira.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/nccr-mageuzi-wataka-rugemalira.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy