Ewura: Bei ya umeme kupungua wakati wowote
HomeHabariKitaifa

Ewura: Bei ya umeme kupungua wakati wowote

Wakala wa Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), umetangaza kuwa wakati wowote kuanzia sasa serikali itapunguza bei...

Serikali kunusuru machinga nchini
Magari ya utalii Tanzania yakataliwa kuingia JKIA
Pinda ashukiwa ndani na nje ya Bunge




Wakala wa Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), umetangaza kuwa wakati wowote kuanzia sasa serikali itapunguza bei ya umeme baada ya gharama za mafuta kupungua katika soko la dunia.

Tanesco inauza ‘uniti’ moja ya umeme kwa Shilingi 306 na pia hutoza tozo la Shilingi 7,000 ambalo halina kuhojiwa wala kupingwa likidaiwa ni la kuendesha shughuli za Ewura, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na kodi ya VAT.

Kaimu Mkurugenzi wa Umeme wa Ewura, Godfrey Chibulunje, alisema wakati wa mkutano wa wadau wakiwamo viongozi vya vyama vya siasa visivyo na wabunge.

Alitoa ufafanuzi huo baada ya viongozi hao kuwabana wataalamu hao na watendaji wa wakala huyo, Shirika la Umeme la Tanesco kueleza kwa nini hawashushi bei za umeme wakati mafuta yameshuka.

Aidha, Chibulunje alisema serikali ipo katika mchakato wa kupitia mwenendo wa kupungua kwa bei ya mafuta kwa lengo la kuangalia namna ya kuwapunguzia mzigo wananchi.

‘’Muda si mrefu wananchi wataona matokeo ya kuanguka kwa bei ya mafuta, tunachokifanya ni kupitia gharama ya ununuzi wa mafuta mazito na kiasi gani wananchi wanaweza kuondokana na mzigo wa kununua umeme,” alisema.

Walihoji pia sababu za kuuza umeme ghali wakati kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL imeshusha bei. Chibulunje alisema hana taarifa kuwa IPTL imepunguza bei ya umeme inaouza Tanesco.

“Kama serikali tulisikia taarifa hizo kwenye vyombo vya habari, tunachojua IPTL inauza umeme kwa bei ya zamani, hizo taarifa ya kushusha hatuna na kama zipo hazijatufikia kiofisi,” alisema Chibulunje.

Alifafanua kwamba kiutaratibu kama kampuni au shirika linataka kupunguza au kupandisha bei ya huduma lazima inawasilisha mapendekezo ofisini kwake kwa ajili ya kufanyia kazi, hata hivyo haikufanyika jambo kama hilo.

Awali, Mwenyekiti wa makatibu wa vyama 12 vilivyoshiriki katika mkutano huo, Ali Kaniki, alisema wanasikitishwa na hali ya wananchi kuendelea kuteseka na kubebeshwa gharama kubwa ya huduma hiyo wakati kuna baadhi ya kampuni zimeanza kushusha bei ya umeme.
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Ewura: Bei ya umeme kupungua wakati wowote
Ewura: Bei ya umeme kupungua wakati wowote
http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2014/10/EWURA.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/ewura-bei-ya-umeme-kupungua-wakati.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/01/ewura-bei-ya-umeme-kupungua-wakati.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy