Serikali kunusuru machinga nchini
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
HomeHabariKitaifa

Serikali kunusuru machinga nchini

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda SERIKALI imeingilia kati manyanyaso wanayopata wafanyabiashara ndogo na mamalishe nchini, kwa kuamua kuun...

Lowassa Ni Moto Wa Kuotea Mbali.....Mamia ya Wachungaji Waandamana Kuelekea Nyumbani Kwake Kumtaka Agombee Urais Huku Wakiwa na Mabango
Lowassa HAKAMATIKI.....Bodaboda, Machinga na Wanafunzi wa Chuo Kikuu UDOM Waandamana Kwenda Kumtaka Agombee Urais.....Wamkabidhi 800,000 ya Kuchukulia Fomu
Simba SC, Azam zaibana Yanga

SERIKALI imeingilia kati manyanyaso wanayopata wafanyabiashara ndogo na mamalishe nchini, kwa kuamua kuunda kikosi cha kiofisi, kitakachohusisha wajasiriamali hao kwa lengo la kukubaliana juu ya maeneo na muda mwafaka wa kuendesha shughuli zao.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliliambia Bunge jana kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imewasilisha mapendekezo hayo kwake, juu ya hatua za kutatua tatizo hilo.

Pinda alisisitiza kwamba wazo hilo la Tamisemi ni jema, na alitaka mkutano kwa ajili ya utekelezaji wake, uanze wiki ijayo ili waweze kuandaa utaratibu mapema iwezekanavyo.

Alisema hayo akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) aliyesema baadhi ya wabunge wamekuwa wakihoji juu ya manyanyaso ya wafanyabiashara wadogo, mama lishe na waendesha pikipiki (bodaboda).

Alisema, lakini kwa kipindi chote Waziri Mkuu amekuwa akitoa maelekezo juu ya tatizo hilo, lakini mamlaka zinazohusika, haziko tayari kutii amri yake. “Je unawaambia nini Watanzania?” alisema Mangungu.

Akijibu, Pinda alisema matatizo yanayokumba wajasiriamali hao ni makubwa na si kwa Jiji la Dar es Salaam pekee, bali nchi nzima hivyo serikali imeamua kutafuta ufumbuzi wa kudumu na dhamira ipo.

“ Jana (juzi) nimepata taarifa kutoka Tamisemi, wanaleta mapendekezo kwangu juu ya mapendekezo ya kutatua tatizo hilo. Katika taarifa yao, wamependekeza kwamba wataunda kikosi cha kiofisi kitakachofanya kazi kupitia makundi ya viongozi wa wamachinga nchini. Watakubaliana nao juu ya maeneo yatakayotumika na muda muafaka wa kufanya shughuli,” alisema.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, kikubwa alichoona katika mapendekezo ya Tamisemi, wametaka suala la usafi katika maeneo yatakayotumika kwa biashara, lipewe kipaumbele.

Alisema wataanza na Jiji la Dar es Salaam kufikia maelewano na vyombo vyote vinavyohusika, vitaeleweshwa juu ya maafikiano hayo kabla ya mkakati huo kusambaa kwenye majiji na miji mingine.

Alisema suala la kutenga maeneo kwa ajili ya biashara kwa siku maalumu, si la Tanzania pekee kwani liko kwenye nchi nyingi.

“Hata nchi za nje wana Sunday markets (masoko ya Jumapili). Hakuna tofauti na hili,” alisema Pinda na kusisitiza kwamba amekubaliana na Tamisemi jambo hilo walipe kipaumbele tofauti kuliko ilivyokuwa awali.

Kwa muda mrefu, katika miji mikubwa nchini kumekuwa na msuguano wa mara kwa mara baina ya mamlaka katika miji husika na wafanyabiashara, kiasi cha kuonekana kama mamlaka husika hufanya unyanyasaji wa makusudi dhidi ya wafanyabiashara hao.

Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali kunusuru machinga nchini
Serikali kunusuru machinga nchini
http://www.habarileo.co.tz/images/resized/images/dini-pinda_300_172.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/serikali-kunusuru-machinga-nchini.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/02/serikali-kunusuru-machinga-nchini.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy