Katibu wa baraza la masuala ya Afrika Mashariki na Utalii Phyllis Kandie Magari ya kubeba watalii yaliyosajiliwa T...
Katibu wa baraza la masuala ya Afrika Mashariki na Utalii Phyllis Kandie alisema fursa iliyoombwa na Tanzania wiki tatu zilizopita kuruhusu mataifa yote kujadili tatizo hilo imekataliwa.
“Mkutano wa kujadili masuala haya haujafanyika,” alisema Bi Kandie.
Taswira ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), Nairobi |
Bi Kandie alisema serikali awali ilidhamiria kutekeleza makubaliano baina ya Kenya na Tanzania mwaka 1985 kuhakikisha biashara sawa kati ya nchi mbili.
KUKATAA KWA TANZANIA
Maamuzi hayo yalivunja makubaliano yaliyokubaliwa baada ya Tanzania kukataa magari yote ya Kenya kuingina nchini.
Makubaliano ya namna ya kuendesha utalii kati ya mataifa mawili yanapaswa kufanyika.
Makubaliano yaliruhusu magari kushusha watalii kwenye vituo muhimu katika mataifa husika ikipingana na makubaliano ya awali ambapo watalii walishushwa mipakani.
Katibu wa baraza, hatahivyo, alitoa matumaini kwamba makubaliano hayo yatajadiliwa tena kuhakikisha ufanyaji rahisi wa biashara kati ya mataifa yote.
COMMENTS