FT: YANGA 0 : 0 RUVU SHOOTINGS Dakika za lala salama Yanga wanatafuta njia ya kufunga goli, lakini mabeki wa Shootings wamesimama...
Dakika za lala salama Yanga wanatafuta njia ya kufunga goli, lakini mabeki wa Shootings wamesimama imara
Dakika +4′ za nyongeza
Dakika 90 zimeshamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake
Dakika ya 89′ kunatokea Sintofahamu baina ya kipa wa Yanga na
mchezaji wa Shootings baada ya Yondani kumfanyia madhambi mchezaji
pinzani
Dakika ya 89′ kunatokea Sintofahamu baina ya kipa wa Yanga na
mchezaji wa Shootings baada ya Yondani kumfanyia madhambi mchezaji
pinzani
Dakika ya 83′ Salvatory Ntebe anaoneshwa kadi nyekundu
Dakika
ya 81′ Rajab Zahiri ameiokoa Yanga katika hatari baada ya mshambulizi
wa Shooting, Abdulrahman Mussa kubaki yeye na kipa na mpira kuwa kona
ambayo haikuzaa matunda
Dakika ya 80′ si Yanga wala Shootings iliyoona lango la mwenzake
Dakika ya 78′ Niyonzima anapiga mpira wa adhabu ndogo kutoka winga ya kulia lakini mabeki wa Shootings wanaokoa
Dakika ya 75′ milango ya timu zote bado ni migumu na Yanga
wanashindwa kutumia kona waliyopata baada ya mabeki wa Shootings kuokoa
Dakika ya 73′ Yanga wanapata kona, lakini kipa Abdallah Rashind ameanguka chini na anatibiwa
Dakika ya 71′ Hussein Javu anaingia kuchukua nafasi ya Coutinho
Dakika ya 68′ Jerome Lambele anaingia kuchukua nafasi ya Mwita Kemalonge
Dakika ya 68′ Mpira umesimama baada ya mchezaji wa Shootings kufanyiwa madhambi
Dakika ya 65′ Msuva anakwenda benchi nafasi yake inachukuliwa na Daniel ‘Danny’ Davis Mrwanda
TAIFA: Dakika ya 61 hakuna timu iliyopata goli kati ya Yanga na Ruvu Shootings..
………………………………………………………………
NDANDA 0 : 2 SIMBA SC
………………..kutoka Mtwara, Elius Maguri anaifungia Simba bao la pili katika dakika ya 52 akipokea pasi ya Danny Sserunkuma.
………………………………………………………………….
Dakika ya 55′ Yahya Tumbo anakwenda benchi kwa upande wa Ruvu Shootings nafasi yake inachukuliwa na Baraka Mtuwi
Dakika ya 51′ bado milango ni migumu
Dakika ya 47′ hakuna timu iliyoona lango baina ya Yanga na Ruvu Shootings
UWANJA WA TAIFA: YANGA 0 : 0 RUVU SHOOTINGS
………………………………………..
HT: STAND UNITED 0 : 1 AZAM FC
Dakika ya 43, Frank Domayo ameifungia goli la kuongoza Azam fc dhidi ya wenyeji Stand United
KUTOKA NAGWANDA SIJAONA MTWARA…Mpira ni mapumziko Simba
wakiwa mbele kwa goli moja lililofungwa na Danny Sserunkuma katika
dakika ya 32 kipindi cha kwanza akimalizia mpira wa kona uliopigwa na
Elius Maguri
…………………………………….
HT: YANGA 0 : 0 RUVU SHOOTINGS
Dakika ya sita ya nyongeza badala ya tano Yanga wamepata kona mbili mfululizo, lakini hazijazaa matunda
Dakika ya mwisho ya nyongeza kumetokea piga nikupige eneo la Shootings, lakini mabeki wanaokoa.
Dakika 45 zimekamilika na mwamuzi anongeza dakika tano za nyongeza
Dakika ya 44 Shootings wamepoteza nafasi nzuri ya kufunga
Dakika ya 40 Msuva anakosa nafasi nyingine baada ya kuwekewa
mpira na Edward Charles. Mpira huo ulitokana na mpira wa kona kufuatia
shuti la Tambwe kuokolewa na kipa Rashid
Dakika ya 39′ Msuva anakosa bao akiwa yeye na kipa
Dakika ya 36′ Yanga wanapata kona ambayo haizai matunda
Dakika ya 33′ Coutinho anapiga mpira wa adhabu ndogo
unaowababatiza mabeki wa Shootings na kumchanganya kipa Rashid, lakini
anajitahidi kuokoa
Dakika ya 25′ Coutinho amekosa bao baada ya kichwa chake
kutoka nje ya lango akiunganisha krosi ya Niyonzima kutoka winga ya
kulia
Dakika ya 24′ hakuna timu iliyoona lango la mwenzake
Dakika ya 19′ Tambwe amefunga goli kwa mkono mwamuzi anakataa na kumuonesha kadi ya njano
Dakika ya 18′ Saimon Msuva anaoneshwa kadi ya njano
Dakika ya 17 mpira umesimama baada ya Msuva kumfanyiwa madhambi mchezaji wa Shootings ambaye yuko chini
Dakika ya 12′ Andrey Coutinho amepiga mpira wa adhabu ndogo ndani ya eneo la 18, lakini mlinda mlango Rashid Abdallah ameokoa
Dakika ya 6′ kipindi cha kwanza Yanga wanagongeana pasi eneo
lao, lakini wanashindwa kuvuka kirahisi eneo la Shootings kutokana na
ulinzi waliowekewa
Dakika ya 4′ Yanga wameanza kwa kasi wakifika mara kadhaa langoni kwa Shootings lakini mipango haijawa sawa
Yanga wamepata kona sekunde kadhaa lakini haijazaa matunda
Mpira umeshaanza hapa uwanja wa Taifa Yanga wakiwa wa kwanza kugusa mpira
Wachezaji wanasalimiana tayari kwa kuanza kipute
Wachezaji wa timu zote wameingia uwanjani tayari kwa kukaguliwa na waamuzi
COMMENTS