Madiwani Nanyamba wajifunza mbinu za kisasa za usimamizi wa miradi jijini Mwanza
HomeHabariTop Stories

Madiwani Nanyamba wajifunza mbinu za kisasa za usimamizi wa miradi jijini Mwanza

Madiwani na viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wamefanya ziara ya siku moja katika Jiji la Mwanza kwa lengo la kujifunza usimamizi w...

Utengenezaji wa mabehewa 264 ya mizigo umekamilika nchini China -TRC
Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 15, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 15, 2024

Madiwani na viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba wamefanya ziara ya siku moja katika Jiji la Mwanza kwa lengo la kujifunza usimamizi wa miradi na mbinu za kuongeza mapato.

Ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za kuboresha utendaji wa halmashauri hiyo iliyopo mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Nanyamba, Mhandisi Mshamu Munde, amesema wamejifunza jinsi Mwanza inavyosimamia miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa mapato, na utunzaji wa mazingira. Amebainisha kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanatumia maarifa hayo kuboresha miradi yao na kufikia lengo la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 3.5 mwaka ujao wa fedha.

Katika ziara hiyo, walitembelea dampo la Buhongwa, kiwanda cha matofali kinachosimamiwa na halmashauri, pamoja na Stendi Kuu ya Nyegezi. Viongozi hao wamevutiwa na namna miradi hiyo inavyoendeshwa kwa ufanisi na kutoa manufaa kwa jamii.

Aidha, Kaimu Mkuu wa Usafi na Mazingira wa Jiji la Mwanza, Desderius Pole, amewataka viongozi wa Nanyamba kuwekeza zaidi katika vyanzo vya mapato na kuendeleza miradi ya kimkakati ili kufanikisha malengo yao ya maendeleo.

Madiwani hao wamesema wanatarajia kutumia maarifa hayo kuboresha miradi kama ujenzi wa soko, dampo, na stendi, pamoja na kukuza vivutio vya utalii Nanyamba. Wameahidi kuleta mabadiliko chanya kwa kutumia uzoefu walioupata Mwanza.

The post Madiwani Nanyamba wajifunza mbinu za kisasa za usimamizi wa miradi jijini Mwanza first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/YLDONCJ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Madiwani Nanyamba wajifunza mbinu za kisasa za usimamizi wa miradi jijini Mwanza
Madiwani Nanyamba wajifunza mbinu za kisasa za usimamizi wa miradi jijini Mwanza
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/12/IMG-20241222-WA0025-950x633.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/madiwani-nanyamba-wajifunza-mbinu-za.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/12/madiwani-nanyamba-wajifunza-mbinu-za.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy