Mtendaji Mkuu TANROADS aipongeza Saccos kwa kutengeneza faida
HomeHabariTop Stories

Mtendaji Mkuu TANROADS aipongeza Saccos kwa kutengeneza faida

Chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS Saccos), kimepongezwa kwa kutengeneza faida n...

Wanawake Wafanyabiashara na Wafanyakazi wamekutana na kujadili kukuza uchumi wao
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo December 31, 2024
Ajali ya ndege ya Korea Kusini yaua watu 179 huku uchunguzi unaendelea

Chama cha ushirika wa Akiba na Mikopo cha Wafanyakazi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS Saccos), kimepongezwa kwa kutengeneza faida na kujadili namna ya kuzigawa kwa wanachama wake.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Japherson Nnko aliyemwakilisha Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Mhandisi Mohamed Besta katika ufunguzi wa mkutano wa 11 wa TANROADS Saccos uliofanyika leo tarehe 23 Novemba, 2024 mkoani Dar es Salaam.

Mha. Nnko amesema utaratibu huo wa kugawana faida kwa mfumo wa gawio unaonesha wazi namna TANROADS Saccos inavyotekeleza misingi ya ushirika na ilivyopitishwa na umoja wa vyama vya ushirika.

Halikadhalika, amewataka kuwaza makubwa katika ukuaji wake ikiwa ni pamoja na kuongeza bidhaa na huduma wanazotoa sasa za kununua hisa, kuweka akiba na mikopo; na pia bidhaa wanazotoa za mikopo mbalimbali ya maendeleo, wa kupumulia, dharura na kusomesha.

Mh. Nnko amesema kwa sasa TANROADS imehamia Dodoma hivyo Saccos inatakiwa kuangalia fursa ikiwemo ya kununua ardhi kwa ajili ya kujenga majengo ya huduma mbalimbali, ikiwemo kumbi za mikutano.

“Kuna viwango vimetajwa katika nafasi za uwakilishi, nisema tusipende kujirudisha nyuma tuwaze mambo makubwa yanawezekana, hivyo tufikirie pakubwa kwa ajili ya maendeleo,” amesisitiza Mha. Nnko.

Awali kabla kuwasilisha hotuba ya mgeni rasmi Kaimu Mtendaji Mkuu, Mhandisi Nnko amepongeza kwa kuwa na wanachama wengi ambapo hadi Novemba 23, 2024 wana takribani waachama 1927 na kuwa na mtaji mkubwa.

“Pia amewataka wanachama kujifunza kuweka akiba ambazo zitawasaidia wakati mwigine kwa matumizi mbalimbali.

Kw aupande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS Saccos, Bw. Meritus Njeama amesema wamepata mafanikio kwa kuongeza hisa kutoka 55,455 zenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwa kila hisa, hivyo kufanya thamani ya hisa zote kuwa shilingi milioni 554,550,000; pia mikopo imetolewa kwa wanachama 551 yenye thamani ya shilingi milioni 4,749,821,000 na kufanya bakaa ya mikopo kwa wanachama kuwa Milioni 7,854,745.23.

Bw. Njeama amesema mafanikio mengine ni kushika nafasi ya 17 kitaifa kati ya vyama 20 bora kwa kuwa na kiwango kikubwa cha bakaa la akiba na amana; pia kushika nafasi ya 20 bora kitaifa katika vyama vya ushirika vyenye bakaa kubwa la mikopo na nafasi ya 20 kitaifa kwa kuwa na kiwango kikubwa cha rasilimali.

Amesema katika uhai wa chama wameweza kuongeza wanachama, kuongezeka kwa faida baada ya kodi, uwekaji mzuri wa hisa na akiba, kuongezja kwa rasilimali na kuongezeka kwa mtaji wa chama.

Hatahivyo, amesema katika mipango ya baadae kwa mwaka 2025 pamoja na changamoto zinazokabiliana na soko, wamedhamiria kuboresha utoaji wa huduma na kutoa elimu kwa wanachama.

Kwa nyakati tofauti washiriki kwenye mkutano huo Mhandisi John Mahenge, Mwenyekiti Tawi la Kilimanjaro na Bi. Rebecca Msenga, Katibu Tawi la Mwanza wameshukuru kwa mkutano huu mkuu, ambao umewezesha kujua mambo mbalimbali yaliyoendeshwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.

The post Mtendaji Mkuu TANROADS aipongeza Saccos kwa kutengeneza faida first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/Filea8v
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mtendaji Mkuu TANROADS aipongeza Saccos kwa kutengeneza faida
Mtendaji Mkuu TANROADS aipongeza Saccos kwa kutengeneza faida
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/11/82e9f1e4-d584-46e6-9b52-df99db060d3e-950x633.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/mtendaji-mkuu-tanroads-aipongeza-saccos.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/11/mtendaji-mkuu-tanroads-aipongeza-saccos.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy