Mkurugenzi mkuu TRC atembelea majeruhi wa ajali ya treni Kigoma
HomeHabariTop Stories

Mkurugenzi mkuu TRC atembelea majeruhi wa ajali ya treni Kigoma

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa  ametembelea majeruhi wa  ajali ya treni mkoani Kigoma na kutangaza kuwa se...

GSM atangaza rasmi kinywaji kipya, Yanga SC apata Shavu la kukitangaza…
Mama mzazi wa Mbunge Halima Mdee, Theresa Mdee afariki Dunia
Habari kubwa Magazetini Kenya leo July 30, 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa  ametembelea majeruhi wa  ajali ya treni mkoani Kigoma na kutangaza kuwa serikali  itagharamia matibabu ya abiria 73 waliojeruhiwa katika ajali ya treni ya abiria iliyoanguka eneo la Lugufu wilaya ya Uvinza usiku wa kuamkia Agosti 28 mwaka huu.

Kadogosa amesema  hayo  alipowatembelea majeruhi katika hospitali ya rufaa ya mkoa kigoma Maweni na hospitali ya wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma ambapo  amesema kuwa pamoja na kugharamia matibabu kwa majeruhi wote pia TRC itawasafirisha majeruhi wote wa ajali hiyo kuendelea na safari zao hadi wanapokwenda.

Akiwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk.Lameck Mdengo amesema kuwa hadi sasa wamebaki wagonjwa wanne kati ya watano waliokuwa wamelazwa hospitalini hapo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa hospitali ya wilaya Uvinza, Dk.David Patrick George amesema kuwa wagonjwa 73 walipokewa hospitalini hapo siku ya ajali na hadi kufikia leo  mchana wakati Mkurugenzi Mkuu anatembelea majeruhi hospitalini hapo walibaki wagonjwa sita ambapo  katika wagonjwa hao  watatu waliomba kuendelea na safari baada ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu hospitalini hapo na wagonjwa watatu watahamishiwa hospitali ya rufaa ya mkoa Kigoma Maweni kwa matibabu zaidi.

Baadhi ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali za rufaa mkoa Kigoma akiwemo Hamida Hamza ambaye ameumia mgongo na mbavu amelishukuru shirika la reli, uongozi wa serikali ya mkoa na waganga katika hospitali za Uvinza na kwa jitihada kubwa walizofanya tangu ajali ilipotokea hadi sasa wanapoendelea na matibabu ambapo hawajadaiwa gharama zozote za matibabu wala chakula.

Hadi sasa hakuna kifo kilichoripotiwa ambapo Kwa majeruhiwa wanne waliopo Hospitali ya Rufaa Maweni wanaendelea na matibabu na vipimo kutazama hali zao zaidi.

The post Mkurugenzi mkuu TRC atembelea majeruhi wa ajali ya treni Kigoma first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/lDcK2W4
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mkurugenzi mkuu TRC atembelea majeruhi wa ajali ya treni Kigoma
Mkurugenzi mkuu TRC atembelea majeruhi wa ajali ya treni Kigoma
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2024/08/IMG-20240829-WA0124-950x634.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mkurugenzi-mkuu-trc-atembelea-majeruhi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2024/08/mkurugenzi-mkuu-trc-atembelea-majeruhi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy