Mkutano Wa 42 Wa Kawaida Wa Baraza La Mawaziri Waendelea Kufanyika Jijini Arusha
HomeHabari

Mkutano Wa 42 Wa Kawaida Wa Baraza La Mawaziri Waendelea Kufanyika Jijini Arusha

  Mkutano wa 42 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha kw...

Chuo Cha IFM Chazungumzia Tukio La Moto Lililotoka Chuoni Hapo
Rais Samia Afanya Uteuzi wa Viongozi Mbalimbali
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo May 21

 


Mkutano wa 42 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaendelea katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha kwa ngazi ya Maafisa Waandamizi.

Mkutano huo ambao unafanyika kwa njia ya mseto (Video na ana kwa ana) pamoja na masuala mengine unatarajiwa kupitia ripoti mbalimbali kama vile; ripoti ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa na Mkutano wa 41 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya, ripoti ya ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ambayo itajumuisha taarifa za Ukaguzi wa Fedha, ripoti ya Mipango na Miundombinu na ripoti ya Sekta za Uzalishaji na Huduma za Jamii.

Mkutano huo  utakaofanyika kwa kipindi  cha siku nne, umeanza katika ngazi ya Maafisa Waandamizi tarehe 8 na 9 Juni 2022, utafuatiwa na Makatibu Wakuu tarehe 10 Juni 2022 na hatimaye tarehe 11 Juni 2022 kuhitimishwa na Mawaziri.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo kwa ngazi ya Maafisa Waandamizi unaongozwa na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen P. Mbundi,  wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kila mwaka, Baraza la Mawaziri la Jumuiya hukutana mara mbili ambapo mkutano mmoja kati ya hiyo hufanyika kabla ya mkutano wa Wakuu wa Nchi  Wanachama wa Jumuiya. Miongoni mwa malengo ya Mikutano ya Baraza la Mawazi ni kuhusianisha maamuzi yanayofikiwa kwenye Mikutano ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya  na majukumu ya utendaji wa kila siku  ya Jumuiya.


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mkutano Wa 42 Wa Kawaida Wa Baraza La Mawaziri Waendelea Kufanyika Jijini Arusha
Mkutano Wa 42 Wa Kawaida Wa Baraza La Mawaziri Waendelea Kufanyika Jijini Arusha
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9jOipXKetTZN3Iz2vr15DTC_MS3W_I6SehV9hJOy_Wn3gwOZDbDtbsgbWpKaHwMLIM8Yn4Tom4vTFa9TNJASMNkuWBQc_nKM4SZvyFaeAlRfQJ1e3d-sFgTGPAlLm8r6Ph4VBvLOnsdq_dv1FrJdxsQV5L8a94U58GVYbIwUpOg54md5yzCQF3AnKeg/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj9jOipXKetTZN3Iz2vr15DTC_MS3W_I6SehV9hJOy_Wn3gwOZDbDtbsgbWpKaHwMLIM8Yn4Tom4vTFa9TNJASMNkuWBQc_nKM4SZvyFaeAlRfQJ1e3d-sFgTGPAlLm8r6Ph4VBvLOnsdq_dv1FrJdxsQV5L8a94U58GVYbIwUpOg54md5yzCQF3AnKeg/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/mkutano-wa-42-wa-kawaida-wa-baraza-la.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/mkutano-wa-42-wa-kawaida-wa-baraza-la.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy