HomeHabariTop Stories

Watu wasiopungua 20 wafariki kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini

Watu wasiopungua 20 wameuawa nchini Sudan Kusini baada ya ndege kuanguka muda mfupi baada ya kupaa Msemaji wa Mamlaka ya anga ya Sudan Kusi...

Watu wasiopungua 20 wameuawa nchini Sudan Kusini baada ya ndege kuanguka muda mfupi baada ya kupaa

Msemaji wa Mamlaka ya anga ya Sudan Kusini, amesema watu 21, wakiwemo raia wa Sudan Kusini na wageni, walikuwa kwenye ndege hiyo iliyokuwa ikitokea jimbo la Unity kwenda mji mkuu wa Juba.

Abiria walikuwa wafanyakazi wa makampuni ya mafuta waliokuwa wanarudi nyumbani baada ya kufanya kazi kwenye visima vya mafuta. Sababu ya ajali bado haijafahamika, lakini serikali ya jimbo la Unity ilisema inafanya kazi na makampuni ya mafuta na kampuni ya ndege kubaini majina ya wahanga.

Ajali za ndege hutokea mara kwa mara nchini Sudan Kusini, kwa sababu mashirika ya ndege hutumia ndege za zamani na zisizo na matengenezo bora.

Nchi hiyo, ambayo ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani, ina mtandao mbovu wa barabara, hivyo wasafiri hutegemea ndege kwa safari ndefu.

The post Watu wasiopungua 20 wafariki kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/6YZCQJf
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Watu wasiopungua 20 wafariki kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini
Watu wasiopungua 20 wafariki kwenye ajali ya ndege Sudan Kusini
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/watu-wasiopungua-20-wafariki-kwenye.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/watu-wasiopungua-20-wafariki-kwenye.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy