Mkutano Wa Nne Wa JPC Ngazi Ya Makatibu Wakuu Wafanyika Jijini Kampala, Uganda
HomeHabari

Mkutano Wa Nne Wa JPC Ngazi Ya Makatibu Wakuu Wafanyika Jijini Kampala, Uganda

Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje wa Tanzania na Uganda wamefungua Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzan...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo September 2, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo September 2, 2024
Picha:Ufunguzi wa mafunzo ya shirikisho la askari wa kike duniani na wasiamizi wa sheria Chicago Nchini marekani


Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje wa Tanzania na Uganda wamefungua Mkutano wa Nne wa Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) kati ya Tanzania na Uganda uliofanyika  tarehe 18 Januari 2022 katika Ngazi ya Makatibu Wakuu jijini Kampala, Uganda.


Akihutubia katika Mkutano huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab ameishukuru serikali ya Uganda kwa mapokezi mazuri sambamba na maandalizi mazuri ya Mkutano.


Pia, akaeleza tangu kumalizika kwa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja kati ya Nchi hizo mbili mwaka 2019, masuala mengi yametekelezwa kwa pamoja katika nafasi mbalimbali na kupitia utaratibu wa Mikutano ya kisekta ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.


”Nchi zetu zinatakiwa kufuatilia utekelezaji katika sekta za ushirikiano kuanzia ngazi ya Wizara, Idara na Taasisi za Seriakali ili  kutatua changamoto na kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano”, alisema Balozi Fatma.


Kwa upande wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje wa Uganda, Bw. Kagiire Waiswa alieleza Mkutano huu unajadili na kutathimini utekelezaji katika sekta za ushirikiano zitakazowasilishwa katika Mkutano Ngazi ya Mawaziri utakaofanyika kesho tarehe 19 Januari 2022.


”Ni imani yangu kuwa majadiliano katika Mkutano huu yatafikiwa muafaka kwa namna bora na yatazingatia ushauri wa kitaalamu kutoka pande zote mbili”, alisema Bw. Waiswa.


Pia akaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta timu ya Wataalamu iliyokamilika na kurahisisha majadiliano katika sekta zote za ushirikiano zilizokubaliwa na Nchi hizo.

Viongozi hao kwa pamoja wameonesha imani kubwa waliyonayo kupitia majadiliano hayo ili kuimarisha ushirikiano katika sekta za Biashara, Uwekezaji, Siasa na Diplomasia, Nishati, Maji na Mazingira, Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Utalii, Afya, Kilimo, Mifugo, Uvivu, na Elimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mkutano Wa Nne Wa JPC Ngazi Ya Makatibu Wakuu Wafanyika Jijini Kampala, Uganda
Mkutano Wa Nne Wa JPC Ngazi Ya Makatibu Wakuu Wafanyika Jijini Kampala, Uganda
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEj66XiA9eUxLPUyxTUrS2QkcADd7nEV_7bs5i05_QYJDLAxZxh1OnpdwEY0LSNe0Ll-z67XV70ac73qMnkb_gKiZTKS3cP4zIucQZLjSJtREtf2sCZh8GiqD8fjNdoVSgndlC4OUp7zjO0kOKQcSv_GApc5iqYR2iHhuP-UxX6pJaRhrseXOvZtXgpCQQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEj66XiA9eUxLPUyxTUrS2QkcADd7nEV_7bs5i05_QYJDLAxZxh1OnpdwEY0LSNe0Ll-z67XV70ac73qMnkb_gKiZTKS3cP4zIucQZLjSJtREtf2sCZh8GiqD8fjNdoVSgndlC4OUp7zjO0kOKQcSv_GApc5iqYR2iHhuP-UxX6pJaRhrseXOvZtXgpCQQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/mkutano-wa-nne-wa-jpc-ngazi-ya-makatibu.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/01/mkutano-wa-nne-wa-jpc-ngazi-ya-makatibu.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy