JITIHADA za vijana wa Azam FC waliokuwa wananolewa na Kocha Msaidizi, Vivier Bahati katika kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Kagame, zi...
JITIHADA za vijana wa Azam FC waliokuwa wananolewa na Kocha Msaidizi, Vivier Bahati katika kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Kagame, ziligonga mwamba jana Agosti 11.
Bao la mapema la Bright Muthalk dk ya kwanza liliwapoteza wawakilishi wa Tanzania, Azam FC waliokubali kwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao hilo.
Kipindi cha pili waliamka Azam FC na kutengeneza majaribio kadhaa na iliwabidi wasubiri mpaka dk ya 67 kupachika bao la usawa kupitia kwa Paul Peter.
Kasi ilizidi kuwa kubwa kwa vijana hao ambapo dk ya 74 nyota wao mwingine Oscar Masai alipachika bao la pili kwa Azam FC.
Bao hilo lilidumu dk mbili pekee kwa kuwa makosa ya safu ya ulinzi yalimpa manufaa Bright tena akapachika bao la usawa dk 76 na kufanya ubao wa Azam Complex kusoma Azam FC 2-2 Big Bullets.
Zilipoongezewa dk 30 hakukuwa na mbabe na Azam FC ilitolewa katika changamoto ya penalti ambaoo ilifunga 2-4 Big Bullets ambao watacheza fainali Jumamosi na Express ambao waliwatoa KMKM.
Bahati amesema kuwa vijana wake walipambana katika kusaka ushindi ila makosa ya kipindi cha kwanza yaliwagharimu na kuwafanya washindwe kushinda mchezo huo.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS