Mataifa matano yenye nguvu kubwa kinyuklia ulimwenguni yameahidi kuzuia ongezeko zaidi la silaha za nyuklia na kusema vita vya nyuklia ha...
Mataifa matano yenye nguvu kubwa kinyuklia ulimwenguni yameahidi kuzuia ongezeko zaidi la silaha za nyuklia na kusema vita vya nyuklia haviwezi kuwa chaguo na ni lazima vizuiwe kwa nguvu zote.
Mataifa hayo yamesema silaha za nyuklia zinatakiwa kutumika kwa ajili ya ulinzi, kuzuia uingiliaji na hata vita.
Ahadi hiyo imetolewa kabla ya mapitio ya kumi na ambayo ni ya karibuni zaidi ya mkataba wa kuzuia kuongezeka kwa silaha za nyuklia ama NPT yaliyopangwa kufanyika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwezi huu, lakini yaliahirishwa hadi baadae mwaka huu.
Taarifa ya pamoja na ya nadra ya mataifa hayo matano yenye nguvu kubwa kinyuklia ulimwenguni ambayo ni China, Ufaransa, Urusi, Uingereza na Marekani imetolewa jana Jumatatu. Kwa pamoja yameahidi kuzuia kuongezeka kwa silaha hizo za nyuklia na kuongeza kuwa wana imani thabiti kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuzuia kusambaa zaidi kwa silaha kama hizo.
Kwenye taarifa hiyo, mataifa hayo yamesema badala yake silaha za nyuklia zinatakiwa kutumika kwa shughuli za ulinzi, kuzuia uingiliaji pamoja na vita.
Mataifa hayo matano ambayo ni wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa yamekubaliana pia kufanya mazungumzo kwa nia njema kuhusiana na hatua madhubuti za kusitisha ushindani wa kuzitengeneza, pamoja na kuzipokonya silaha hizo, lakini pia mkataba wa utekelezwaji wa hatua hizo chini ya udhibiti mkali wa kimataifa.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS