Dirisha dogo la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite limefunguliwa r...
Dirisha dogo la usajili kwa klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite limefunguliwa rasmi leo Desemba 16, 2021 na kutarajiwa kufungwa Januari 15, 2022.
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF zinasema kuwa katika kipindi hicho klabu zinatakiwa kutumia kufanya na kukamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa.
Klabu yoyote itakayokuwa na changamoto inatakiwa kuwasiliana na na TFF Idara ya Mashindano.
TFF imeongeza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa kwa dirisha, hivyo ni vyema klabu kukamilisha usajijili na uhamisho kwa wakati.
Credit: MPEKUZI
Thanks for your time please share with your friends
COMMENTS