Rais Samia- Miaka 60 ya uhuru, Kiswahili kimekua kimataifa.
HomeHabari

Rais Samia- Miaka 60 ya uhuru, Kiswahili kimekua kimataifa.

Na. John Mapepele Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru leo Disemba...

Mabula Atatua Mgogoro Wa Mpaka Kati Ya Newala Na Masasi
Dk. Mwinyi Umefika Wakati Wa Kuunda Tume Kupambana Na Udhalilishaji.
Waziri Ndugulile Aendesha Kikao Cha Mapato Na Matumizi Ya Wizara Na Taasisi Zake


Na. John Mapepele
Rais wa Jamhuri ya Tanzania. Mhe, Samia Suluhu Hassan kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru leo Disemba 9, 2021 amesema Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye lugha ya Kiswahili.

Rais Samia ameyasema haya jana usiku Disemba 8, 2021 jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia wananchi ambapo alieleza pamoja na mambo mengine mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania.
 

“Nchi nyingi zinatumia lugha za kigeni kama lugha za mataifa yao zinazowaunganisha, inapendeza kuona kuwa tunatimiza miaka 60 tukiwa wamoja wenye utambulisho mmoja na lugha moja ya Kiswahili inayoendelea kupata umaarufu kimataifa   siku hadi siku”. Amefafanua Rais Samia.

Amesema wakati Tanzania ilipopata uhuru Kiswahili haikuwa lugha inayozungumzwa na watu wote ndani ya Tanganyika bali kizazi kilichofuata baada ya uhuru walijifunza kiswahili shuleni. Hii inafanya nchi kuwa kati ya nchi chache zenye lugha ya taifa yenye asili ya nchi husika.

Ameongeza kuwa katika miaka 60 Tanzania imefanikiwa kushawishi Kiswahili kuwa moja ya lugha rasmi zinazotumika  katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika na Umoja wa Afrika.
 

Amesema, Shirika la Umoja wa Mataifa Sayansi na Elimu (UNESCO) limepitisha azimio la kutenga siku ya tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya Kiswahili duniani ambapo amesema azimio hilo linaifanya lugha ya Kiswahili kuwa kuwa ya kwanza katika bara la Afrika kutambuliwa na kutengewa siku yake rasmi.
 

Akiongea na Waandishi wa Habari hivi karibuni, mara baada ya UNESCO kupitisha rasmi azimio hilo Waziri mwenye dhamana ya Utamaduni nchini, Mhe. Innocent Bashungwa aliwataka wadau mbalimbali wa Kiswahili nchini kuendelea kutumia lugha hiyo ili iendelee kukua duniani.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Rais Samia- Miaka 60 ya uhuru, Kiswahili kimekua kimataifa.
Rais Samia- Miaka 60 ya uhuru, Kiswahili kimekua kimataifa.
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjzk6OHPF05Y2VzYV4he82EymjALGIwvaFxlffgsl2WG4ZGM6PuWvGLpVMkZzh3TtT-VTfVunfngmoPWfUAFSDOgRUuqC8DUUGvsCDwmHKgIbd7glKLQlHx1842Cp_8HIyGzXBSIRJheIV4DOv4byimxfkwBVBeJkq7qURqcW0xeGloQdoR9qgFonmiJA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjzk6OHPF05Y2VzYV4he82EymjALGIwvaFxlffgsl2WG4ZGM6PuWvGLpVMkZzh3TtT-VTfVunfngmoPWfUAFSDOgRUuqC8DUUGvsCDwmHKgIbd7glKLQlHx1842Cp_8HIyGzXBSIRJheIV4DOv4byimxfkwBVBeJkq7qURqcW0xeGloQdoR9qgFonmiJA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/rais-samia-miaka-60-ya-uhuru-kiswahili.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/12/rais-samia-miaka-60-ya-uhuru-kiswahili.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy