Walengwa Wa Tasaf Watakiwa Kutotumia Fedha Wazozipata Katika Anasa
HomeHabari

Walengwa Wa Tasaf Watakiwa Kutotumia Fedha Wazozipata Katika Anasa

 NA TIGANYA VINCENT Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amewasa walegwa wa ...


 NA TIGANYA VINCENT
Naibu Wazari Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amewasa walegwa wa Mpango wa Kusuru Kaya Masikini (TASAF) kuacha kuzitumia fedha wanazopatiwa kwa matumizi ya starehe na anasa.


Kauli hiyo imetolewa jana wakati alipokuwa akizungumza na walegwa wa Mpango huo katika Kijiji cha Kinamagi wilayani Uyui Mkoani Tabora


Alisema kwamba fedha wanazopatiwa wanapaswa kuzitumia kwa ajili ya kuboresha maisha yao na kusonga mbele ili maisha yao yawe tofati na wakati ambapo walikuwa hajaanza kupata fedha hizo.


Ndejembi alisema Walengwa wanatakiwa kutumia fedha wanazopatiwa na Serikali ya Awamu ya Tano kutoka hapo walipo  na kwenda ngazi nyingine ambayo itawawezesha kuwavusha kutoka katika umaskini na kupata maendeleo.


“Mnatakiwa kujipima katika kipindi cha madirisha 24 ya TASAF , fedha mlizopatiwa zimewasaidiaje…wapo walengwa katika kipindi hicho wameweza kufanya mambo makubwa …. ni vema mkajiuliza TASAF itakamalizika utakuwa umepiga hatua gani? alisema

Alisema kwamba kila mlengwa anatakiwa kutumia fedha hizo vizuri kwa ajili ya kuisaidia familia kwa kuwapeleka watoto shule,klinick na kujiwekea akiba .

Aidha aliwataka maafisa ugani kuhakikisha wanatoka maofisini na  kwenda kutoa elimu kwa walegwa na  Tasaf ili kuweza kufanya ufagaji ulio bora.

Awali Katibu Tawala Msaidizi(Mipango na Uratibu ) mkoani Tabora Rukia Manduta alimweleza Naibu Waziri huyo kuwa toka mwaka 2015 hadi 2020 jumla ya shilingi bilioni 39.9 zimetolewa kwa walengwa.

Alisema kiasi hicho cha fedha kimewawezesha lipata  elimu ya Ujasiriamali inayotolewa na wataalamu katika kila dirisha la uhaulishaji, lengo ni kuwasaidia kaya hizo kuibua miradi midogo itakayo wawezesha kuongeza kipato.

Manduta alisema hatua inesaidia Kaya za walengwa kupata uhakika wa chakula cha kuwafanya wapate mlo mara tatu

Manduta aliongeza kuwa sanjari na hayo jumla ya walengwa 26,193 wamejiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF).

Alisema kuwa kaya za walengwa zilizopo kwenye mpango zimeweza kuanzisha miradi midogo midogo kama vile Mama Lishe, kilimo cha bustani, ufugaji wa Kuku, Mbuzi, Ng’ombe, Nguruwe, Kondoo pamoja na Ufugaji wa Nyuki.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Walengwa Wa Tasaf Watakiwa Kutotumia Fedha Wazozipata Katika Anasa
Walengwa Wa Tasaf Watakiwa Kutotumia Fedha Wazozipata Katika Anasa
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKDt3IIi0QsOZLc6qgIeKVlpDh1XLz8qaRoRkI1ImgVS2Sj92CN9W0PyU8O3UJGk4nDqX5QP9L9dtEBVBPiNwvjmhtCmTTRYmXCbdvw7xvWE_inYwc8bBL79wfx02JWx6cZzgQXKS7N-Vz/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKDt3IIi0QsOZLc6qgIeKVlpDh1XLz8qaRoRkI1ImgVS2Sj92CN9W0PyU8O3UJGk4nDqX5QP9L9dtEBVBPiNwvjmhtCmTTRYmXCbdvw7xvWE_inYwc8bBL79wfx02JWx6cZzgQXKS7N-Vz/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/walengwa-wa-tasaf-watakiwa-kutotumia.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/01/walengwa-wa-tasaf-watakiwa-kutotumia.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy