Serikali Yadhamiria Kila Mtanzania Kuwa Na Anwani
HomeHabari

Serikali Yadhamiria Kila Mtanzania Kuwa Na Anwani

 Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha kwamba kila Mtanzania...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo June 28, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 28, 2024
MNEC CCM Rukwa atofautiana na Serikali kufungwa uvuvi Ziwa Tanganyika


 Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anakuwa na anwani za makazi ifikapo mwaka 2022.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt.  Zainab Chaula katika semina ya kujenga uelewa kwa Makatibu Tawala wa Mikoa ya Tanzania Bara kuhusu utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi.

"Tunatarajia kufikisha mawasiliano mpaka vijijini, tunataka nchi nzima iwe na anwani ya makazi," amedokeza Dkt. Chaula.

Aidha, amehabarisha kuwa baadhi ya faida za kuwa anwani za makazi ni kurahisisha ukusanyaji kodi, kuwezesha biashara mtandao na kuimarisha ulinzi na usalama.

Awali, akifungua semina hiyo, Katibu Mkuu wa  Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof. Riziki Shemdoe amesema Serikali za Mikoa zina majukumu ya kusimamia utekelezaji wa anwani za Makazi kwenye maeneo yao

"Serikali yetu ya Tanzania kupitia Sera ya Posta ya mwaka 2003 imeimarisha mifumo ya anwani za makazi inayoundwa na barabara, njia na namba za nyumba," amebainisha.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mary Makondo amesisitiza ushirikiano ili kufikia malengo kwa kuwa moja ya manufaa ya anwani hizo ni kuwezesha na kufanikisha utambuzi wa majengo na viwanja vilivyopo ili kurahisisha kazi ya mipango miji na utekelezaji wa majukumu ya kiuchumi na kijamii kwa Serikali na wananchi kwa ujumla

"Naamini tutaendelea kushirikiana katika kujenga nchi yetu na kuwahudumia Watanzania," ametanabaisha Bi. Makondo

Ibara ya 61(m) ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020-2025 inaielekeza Serikali iliyopo madarakani kuhakikisha anuani za makazi zinawekwa nchini ili kurahisisha upatikanaji, utoaji na ufikishishaji wa huduma mbali mbali kwa wananchi

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Serikali Yadhamiria Kila Mtanzania Kuwa Na Anwani
Serikali Yadhamiria Kila Mtanzania Kuwa Na Anwani
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEg9XGmpzsAad283tnZaIfNMwty7F6WGQl-g7GyrK34i0M0ZJkxEB3PS7CZclCWyhhocGyudCxoX4w714hjTUaJsWJsAkjg6KqzUY6aQBGgDYfMS4Cc9i7adi7JMMb-sQLWlNYLJwByQmAhDfJzx4iVVWoTAqsS8w3N5fjK-GC13lqUUAArsURM_23Nicg=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEg9XGmpzsAad283tnZaIfNMwty7F6WGQl-g7GyrK34i0M0ZJkxEB3PS7CZclCWyhhocGyudCxoX4w714hjTUaJsWJsAkjg6KqzUY6aQBGgDYfMS4Cc9i7adi7JMMb-sQLWlNYLJwByQmAhDfJzx4iVVWoTAqsS8w3N5fjK-GC13lqUUAArsURM_23Nicg=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/serikali-yadhamiria-kila-mtanzania-kuwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/serikali-yadhamiria-kila-mtanzania-kuwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy