BEKI mahiri wa kikosi cha Chelsea, Thiago Silva anaandaliwa mkataba mpya ikiwa ni siku chache baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa...
BEKI mahiri wa kikosi cha Chelsea, Thiago Silva anaandaliwa mkataba mpya ikiwa ni siku chache baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Chelsea ilisepa na taji hilo baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa fainali iliyochezwa Uwanja wa Drago,Porto, Ureno.
Beki huyo mwenye miaka 36 anajiandaa kupewa mkataba mpya wa mwaka mmoja ambao utamfanya asalie ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Thomas Tuchel.
Taarifa zimeeleza kuwa atapewa mkataba wa muda mfupi kabla ya michuano ya Euro kuanza.
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS