Majaliwa: Tanapa, Wadau Wa Utalii Shirikianeni Kuitangaza Rubondo
HomeHabari

Majaliwa: Tanapa, Wadau Wa Utalii Shirikianeni Kuitangaza Rubondo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ishirikiane na wadau wa masuala ya utalii ukiwemo uongozi wa k...


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ishirikiane na wadau wa masuala ya utalii ukiwemo uongozi wa kambi ya kupokea watalii ya Asilia kuitangaza hifadhi ya kisiwa cha Rubondo.

Ameyasema hayo jana (Ijumaa, Oktoba 15, 2021) wakati akizungumza na baadhi ya watumishi wa TANAPA pamoja na wa kambi ya Asilia Rubondo akiwa katika ziara fupi ya kuhamasisha utalii katika hifadhi ya Kisiwa Rubondo, Geita.

Amesema ili sekta hiyo iweze kupata tija uongozi wa TANAPA unapaswa kuwa karibu na wadau wa masuala ya utalii. “Endeleeni kuwasikiliza na kushirikiana nao katika kutatua changamoto zinazowakabili ili kuongeza idadi ya watalii.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ameupongeza uongozi wa kampuni ya Asilia kwa uwekezaji wake katika sekta ya utalii nchini na ameusisitiza uendelee kupanua wigo ili kukuza sekta hiyo na kuongeza tija.

Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA Kanda ya Magharibi, Martine Loibooki amemshukuru Waziri Mkuu kwa hatua yake ya kuhamasisha utalii katika hifadhi ya Rubondo na kwamba watayafanyia kazi maelekezo yote aliyoyatoa.

Hifadhi ya Kisiwa cha Rubondo ina ukubwa wa kilometa za mraba 457, iko kaskazini magharibi mwa Tanzania ndani ya ziwa Victoria ziwa ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani. Hifadhi hiyo inaundwa na visiwa vidogo 11 kikiwemo na kisiwa cha ndege.

Kisiwa cha Rubondo ndilo eneo pekee katika ziwa victoria lenye mazalia ya samaki yaliyohifadhiwa kisheria. Samaki wanaopatikana katika kisiwa hicho ni pamoja na  sato na sangara ambao wanaweza kukua hadi kufikia uzito wa hadi kilo 100.

Fukwe za kisiwa hiki ni miongoni mwa makazi ya pongo na nzohe. Aidha hifadhi hii ni maskani makuu ya mamba, ndege na samaki kama zumbuli, chechele na taisamaki, mbali na ndege hao kisiwa hiki ni makazi ya aina nyingine nyingi ya ndege wa majini na mimea kadhaa ambayo hutoa harufu nzuri ya kuvutia.

Wanyama wakazi wa hifadhi ya Rubondo ni pamoja na viboko, pongo, nzohe, fisi maji, mamba na pimbi wanashirikiana makazi na wanyama waliohamishiwa katika hifadhi hiyo kama sokwe, tembo, mbega weusi na weupe na twiga.

Pia, aina nyingine ya utalii inayofanyika katika hifadhi hiyo ni pamoja na uvuvi wa samaki wa kitalii.(sport fishing).


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Majaliwa: Tanapa, Wadau Wa Utalii Shirikianeni Kuitangaza Rubondo
Majaliwa: Tanapa, Wadau Wa Utalii Shirikianeni Kuitangaza Rubondo
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjVeiuTf2H333sSUM44BosOcMRheJ1NuAQiEXBR6EqkrbeuWhNxADHTACMflClJy29lZaWubtKq39l09dDCNujYV0G8cYLq1g3oVWtdDiEq4rXN02Z60HJNm1ffNQctNk90jv-eKof-RF5ZOyDTcRkXYQpmN62r6XdPCzwq6s5IZgTOq86a2u5dqH__aQ=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEjVeiuTf2H333sSUM44BosOcMRheJ1NuAQiEXBR6EqkrbeuWhNxADHTACMflClJy29lZaWubtKq39l09dDCNujYV0G8cYLq1g3oVWtdDiEq4rXN02Z60HJNm1ffNQctNk90jv-eKof-RF5ZOyDTcRkXYQpmN62r6XdPCzwq6s5IZgTOq86a2u5dqH__aQ=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/majaliwa-tanapa-wadau-wa-utalii.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/majaliwa-tanapa-wadau-wa-utalii.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy