TAAWANU yatoa msaada wa vitanda vya kisasa zahanati ya Kyerwa,yagawa mitungi ya gesi
HomeHabariTop Stories

TAAWANU yatoa msaada wa vitanda vya kisasa zahanati ya Kyerwa,yagawa mitungi ya gesi

Taasisi ya Taawanu Islamic Foundation chini ya Mkurugenzi wake wa Kimataifa Hajjat Zahra Dattan (zaradattani on Instagram) imeendelea na zoe...

Taasisi ya Taawanu Islamic Foundation chini ya Mkurugenzi wake wa Kimataifa Hajjat Zahra Dattan (zaradattani on Instagram) imeendelea na zoezi la ugawaji wa vitanda vya kisasa ambapo leo ilikuwa ni zamu ya Wilaya ya Kyerwa iliyopo Mkoani Kagera.

Kiongozi huyo wa Kimataifa akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Taawanu Tanzania na Afrika Sheikh Hashimu Kamugunda pamoja na Viongozi wengine wa Taasisi hiyo ngazi ya Mkoa na Taifa wamefika katika Wilaya ya Kyerwa kwenye zahanati ya Katera kwa ajili ya kutoa msaada wa vitanda kwa ajili ya kuongeza nguvu ya utoaji huduma katika zahanati hiyo.

Akiongea kwa niaba ya taasisi hiyo Hajjat Zahra amesema kuwa wametoa msaada huo baada ya kupokea maombi kutoka kwa wadau ambao waliona zoezi la uzinduzi wa ugawaji wa vitanda 60,000 Kitaifa ndo akaamua afike katika zahanati hiyo ya Serikali iliyojengwa kwa mchango wa wananchi na serikali kwa ajili ya kukabidhi vitanda hivyo pamoja na kuangalia ni namna gani wanaweza kusaidia upande mwingine kwa kushirikiana na serikali ili wananchi waendelee kupata huduma iliyo bora.

Aidha Hajjat Zahra amewaomba wasimamizi na wananchi watakaotumia vitanda hivyo kuvitunza vizuri ili viweze kudumu kwa muda mrefu na kuwasaidia walio wengi.

Sambamba na hilo amekabidhi mitungi ya gesi kwa baadhi ya akina mama wa eneo la Katera ikiwa ni hamasa ya kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia ambayo itawaepusha na changamoto nyingi za Kiafya.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa,Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Daktari Lewanga Msafiri Mandari ameshukuru taasisi ya TAAWANU kwa msaada mkubwa walioutoa katika Wilaya hiyo huku akisema kuwa vitanda walivyovipokea ni vya kisasa na kipekee kabisa ndani ya Wilaya yao kwani ndo mara ya kwanza kupokea vitanda vyenye muundo kama huo na anaamini vitawasaidia kupunguza uchovu kwa watoa huduma pamoja na wauguzi kwani vinatumia teknolojia ya kisasa

   

The post TAAWANU yatoa msaada wa vitanda vya kisasa zahanati ya Kyerwa,yagawa mitungi ya gesi first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/kSyNwlJ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: TAAWANU yatoa msaada wa vitanda vya kisasa zahanati ya Kyerwa,yagawa mitungi ya gesi
TAAWANU yatoa msaada wa vitanda vya kisasa zahanati ya Kyerwa,yagawa mitungi ya gesi
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250110-WA0024-950x534.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/taawanu-yatoa-msaada-wa-vitanda-vya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/taawanu-yatoa-msaada-wa-vitanda-vya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy