Waziri Jafo akutana na Wakazi wa Engaruka
HomeHabariTop Stories

Waziri Jafo akutana na Wakazi wa Engaruka

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amekutana na wananchi wa Engaruka katika zoezi la uhamasishaji kuelekea ulipaji wa fidia ...

BVR Kits 4,257 kuboresha daftari Shinyanga na Mwanza
Habari kubwa Magazetini Kenya leo August 21, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo August 21, 2024

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amekutana na wananchi wa Engaruka katika zoezi la uhamasishaji kuelekea ulipaji wa fidia kwa wakazi wa maeneo ambapo serikali inatarajia kulipa kiasi cha shilingi bilioni 14.4 kwa wananchi wanaotarajia kupisha utekelezaji wa mradi wa maendeleo wa Engaruka, Monduli-Arusha.

Akizungumza mbele ya viongozi wa Serikali, wananchi, na waandishi wa habari, Dkt. Jafo alisisitiza dhamira ya Serikali ya awamu ya sita kuhakikisha fidia inalipwa kwa uwazi, haki, na kwa kuzingatia thamani halisi ya mali za wananchi.


Waziri alisisitiza kuwa Serikali imehakikisha kuwa jumla ya wafidiwa 595 watalipwa fidia kwa kiwango kinacholingana na tathmini iliyofanyika. Alieleza kuwa hakuna mwananchi atakayedhulumiwa au kupunjwa malipo.

Ili kuhakikisha matumizi bora ya fedha za fidia, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na taasisi nyingine za kifedha kama UTT-AMIS, NEEC, NMB, na CRDB, imeandaa semina za kuwaelimisha wananchi kuhusu matumizi sahihi ya fedha hizo. Waziri aliwasihi wanufaika wote kushiriki katika semina hizo.

Waziri alieleza kuwa mradi wa uchimbaji wa madini ya Magadi Soda unaotarajiwa kuanza mara baada ya ulipaji fidia, utatoa ajira kwa wananchi wa eneo husika na kuchangia ukuaji wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Dkt. Jafo alihitimisha kwa kuwataka wananchi wa Engaruka kushirikiana kwa karibu na Serikali ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa bila changamoto.

“Serikali iko nanyi, na dhamira yetu ni kuona kila mmoja wenu anapata haki yake. Tushirikiane kuhakikisha mafanikio ya pamoja,” alisisitiza

The post Waziri Jafo akutana na Wakazi wa Engaruka first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/q4dnBJr
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri Jafo akutana na Wakazi wa Engaruka
Waziri Jafo akutana na Wakazi wa Engaruka
https://millardayo.com/wp-content/uploads/2025/01/a1a378da-835f-4e9e-8834-b5616a7a2109-950x634.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/waziri-jafo-akutana-na-wakazi-wa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/waziri-jafo-akutana-na-wakazi-wa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy