YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOTEZA MBELE YA WANAIJERIA KWA MKAPA
HomeMichezo

YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOTEZA MBELE YA WANAIJERIA KWA MKAPA

  BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United,  uongozi wa timu hiyo umew...

SIMBA YATUMIA MBINU ZA YANGA KUMNASA STRAIKA, NDANI YA CHAMPIONI JUMAMOSI
MAKAMBO ABAINISHA KUWA AMEKUJA KUCHUKUA MAKOMBE
UCHAGUZI WA TFF KILA KITU KINAKWENDA SAWA

 


BAADA ya kikosi cha Yanga kupoteza katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers United,  uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa bado una nafasi ya kupata matokeo katika mchezo wa marudio.


Katika mchezo uliochezwa jana Septemba 12, baada ya dakika 90, ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 0-1 Yanga jambo lililowapa maumivu mashabiki pamoja na Watanzania kiujumla.


Bao pekee la ushindi lilipachikwa na Moses kwa kichwa akiwa ndani ya 18 baada ya kipa namba moja wa Yanga, Diarra Djigui kutoka kidogo katika eneo lake.

Haji Manara,  Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kuna dakika 90 za kupambana.

"Tunazo dakika 90 nyingine za kupambania timu yetu, chini ya jua hili hakuna kisichowezekana. Tupeane pole kwa matokeo lakini tusikate tamaa," 


Katika mchezo wa jana Septemba 12 rekodi zinaonyesha kuwa Yanga ilipiga jumla ya kona 7 huku Rivers United wakipiga kona moja na Yanga ilipiga jumla ya mashuti 13 na ni moja lililenga lango huku Rivers United ikipiga mashuti 11 na ni mawili yalilenga lango.

Kibarua kikubwa ni kwenda kushinda mabao zaidi ya mawili kwa sababu wapinzani wao wanafaida ya bao la ugenini.

Mchezo wao wa marudi unatarajiwa kuchezwa Septemba 18 nchini Nigeria na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa hakuna mwenye uhakika wa kusonga mbele kwa wakati huu mpaka dakika hizo 90 zitakapomeguka.



Credit: SALEH JEMBE

Please subscribe to get all sports news instantly
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOTEZA MBELE YA WANAIJERIA KWA MKAPA
YANGA WATOA TAMKO BAADA YA KUPOTEZA MBELE YA WANAIJERIA KWA MKAPA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3_wc3iKgxzeofYOnLoENCeqxnNl-baIN4HQx4y_Vc-MG-BWJ9NHNkF9MQ8Lt2xmTSmj-fy1ObT5F7Tl63TzTX14Jv4sv-NZXNQLLV3tZA_SgDrdx27dtiTkFHxwYAeYyOdNcUyyq1_jAd/w640-h510/Screenshot_20210913-053812_Instagram.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh3_wc3iKgxzeofYOnLoENCeqxnNl-baIN4HQx4y_Vc-MG-BWJ9NHNkF9MQ8Lt2xmTSmj-fy1ObT5F7Tl63TzTX14Jv4sv-NZXNQLLV3tZA_SgDrdx27dtiTkFHxwYAeYyOdNcUyyq1_jAd/s72-w640-c-h510/Screenshot_20210913-053812_Instagram.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/yanga-watoa-tamko-baada-ya-kupoteza.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/09/yanga-watoa-tamko-baada-ya-kupoteza.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy