Haji Manara Afunguka Mambo Mazito Baada ya Kuondoka Simba
HomeHabari

Haji Manara Afunguka Mambo Mazito Baada ya Kuondoka Simba

Aliyekuwa msemaji wa Simba Haji Manara amevunja ukimya na kueleza sababu zilizomtoa klabuni hapo na nafasi yake kupewa Ezekiel Kamwaga. M...

BREAKING: Wanafunzi 37,731 Wapangiwa Mikopo Ya Tzs 99.9 Bilioni Katika Awamu Ya Kwanza.....Bofya Hapa
Serikali yaikabidhi SUMA JKT shamba la bil. 152/-
Watanzania 940,507 Wapokea Chanjo Ya Jansen

Aliyekuwa msemaji wa Simba Haji Manara amevunja ukimya na kueleza sababu zilizomtoa klabuni hapo na nafasi yake kupewa Ezekiel Kamwaga.

Manara ambaye alihudumu katika timu hiyo kwa zaidi ya miaka sita ameeleza sababu za kutolewa katika nafasi hiyo huku akitaja ni sababu za kibiashara na umaarufu.

Alisema kuwa licha ya kufanya kazi kwa miaka sita katika timu hiyo bila mkataba ila alijitolea vya kutosha kutokana na mapenzi yake kwenye klabu hiyo licha ya kudai kupewa tuhuma alizodai kuwa hazipo.

“Nimefanya kazi ya kujitolea kwenye hii klabu mpaka kufikia hatua ya kusafiri kwa gharama zangu mwenyewe bila hata kupewa na uongozi, hii ni kuonyesha kabisa ni jinsi gani uongozi wa sasa umekuwa ukinifanyia vitu vya kinyama na nisivyotarajia.

“Sina mkataba kwa miaka sita watu wanakuja wanapewa mikataba mie naachwa, sina promotion, laki saba hiyo hiyo imesimama kama mbuyu tangu 2015, nilikubali kwa sababu ni Simba yangu. Naipenda hii klabu namwachia nani?

“Wakati Senzo anakuja kwa mara ya kwanza, alinifuata na kuniambia amepewa kazi ya kunifukuza Mimi kazi, lakini Senzo alihoji kwanini nimfukuze bila sababu?

“Kifupi walimleta Senzo ili atekeleze matakwa ya wakubwa ila Senzo alisimama imara sana, alipinga kufanya kitu bila kukichunguza ndicho kilichomuondoa Simba.

“Simba inacheza nje ya Dar, msemaji wa timu sikatiwi tiketi. Naenda kwa kujitegemea nauli na hoteli. Hadi mechi za nje ya nchi. Nilishawahi kwenda South Africa kwa nauli yangu klabu ilishindwa kunilipia hata hotel, Nikalala kwenye kochi.

“Shida zote nilizopata na Simba, hawa watu hawaniheshimu, hawana mkataba na mimi. Majungu yote wananifanyia sasa leo wananipa jungu jipya la kuhujumu yani mimi nikahujumu Simba? Nahujumu vipi naenda kwenye camp ya Yanga? Nawaambiaje?

“Kuna siku Mohammed Dewji ‘MO’ alininipigia simu akaniambia watu wananilalamikia kuwa wewe umekuwa maarufu kunizidi mimi. Nikamwambia mie nitafanyeje? Nitawazuia watu? Kwani najipa mwenyewe umaarufu? Akaniambia watu wanasema tukutoe nikamwambia nitoeni

“Kwa nini leo sipo Simba? Sababu ni mbili, biashara na umaarufu. Haji ameathirika na hayo mambo mawili. Ndiyo maana unasikia inarudiwa mara nyingi kwamba hakuna mtu mkubwa zaidi ya klabu, lini mimi nimesema ni mkubwa kuliko klabu?” Amesema Manara



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Haji Manara Afunguka Mambo Mazito Baada ya Kuondoka Simba
Haji Manara Afunguka Mambo Mazito Baada ya Kuondoka Simba
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVuDYyP7jNut-NatzEc33ChUHcLiuk0UkibhGRcLsAQqie8kImbZxzE7-zzy__AzalSXLftt9QUxHwwcc3amDLD7Kx9CEEEoHsgGM_v7fp_gYiwe7neDc4uG6B27-ECSJHfvuaFIQOG2Wp/s0/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVuDYyP7jNut-NatzEc33ChUHcLiuk0UkibhGRcLsAQqie8kImbZxzE7-zzy__AzalSXLftt9QUxHwwcc3amDLD7Kx9CEEEoHsgGM_v7fp_gYiwe7neDc4uG6B27-ECSJHfvuaFIQOG2Wp/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/haji-manara-afunguka-mambo-mazito-baada.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/08/haji-manara-afunguka-mambo-mazito-baada.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy