Watanzania 940,507 Wapokea Chanjo Ya Jansen
HomeHabari

Watanzania 940,507 Wapokea Chanjo Ya Jansen

Na Ahmed Sagaff – MAELEZO Watanzania 940,507 wamepokea chanjo ya Jansen ikiwa ni asilimia 88.9 ya chanjo zote 1,058,400 za aina hiyo zi...

Askofu Gwajima na Jerry Slaa waitwa kamati ya maadili ya Bunge
Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo August 22
Rais Samia Awaapisha Mabalozi Aliowateua ....Awaasa kustawisha uhusiano baina ya Tanzania na Mataifa mengine


Na Ahmed Sagaff – MAELEZO
Watanzania 940,507 wamepokea chanjo ya Jansen ikiwa ni asilimia 88.9 ya chanjo zote 1,058,400 za aina hiyo zillizotolewa na Serikali ya Marekani kupitia mpango wa COVAX FACILITY.
 

Hayo yamesemwa leo jijini Mwanza na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa alipokuwa akitoa taarifa ya kazi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

“Shehena ya chanjo 1,065,000 aina ya Sinopharm zilizokuja wiki iliyopita kutoka China zimeanza kusambazwa katika Halmashauri na Mikoa yote nchini na zoezi la uchanjaji linaendelea,” amefahamisha Msigwa.
 

Pamoja na hilo, amehabarisha kuwa Tanzania inatarajia kupokea chanjo zingine aina ya Pfizer dozi 500,000 mwishoni mwa mwezi huu wa kumi kutoka COVAX FACILITY.
 

“Na dozi hizi ni sehemu ya Dozi Milioni 3.7 za chanjo aina ya Pfizer ambazo nchi yetu itazipata kwa awamu kutoka COVAX Facility, tayari hivi navyoongea majokofu ya baridi kali 14 yenye uwezo wa kuhifadhi chanjo zote Milioni 3.7 yameshafungwa pale jijini Dar es Salaam.
 

“Kupitia hii COVAX FACILITY tunatarajia kupata dozi Milioni 11.8 na pia kuna juhudi nyingine za kupata chanjo zinazoendelea ili kutimiza lengo letu la kutoa chanjo kwa asilimia 60 ya Watanzania wote,” ameeleza Msigwa.
 

Sambamba na hayo, amewataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (UVIKO-19) ambazo ni uvaaji barakoa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kuepuka misongamano, kukaa umbali wa meta moja au zaidi, kufanya mazoezi, na kula lishe bora.




Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Watanzania 940,507 Wapokea Chanjo Ya Jansen
Watanzania 940,507 Wapokea Chanjo Ya Jansen
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEg8Nloimfe6zD2aWpykEvsUGYBXjnvvoNHFknrBTbHk4jLnXnavPpjwy-Bnv3me1iSTexR2Ji07fk-9XbePE-WYPNpMZnYjtJy0kWdvza3ukbHFpLhu2u6moK1V9BqKDG5kgEkv2eh-wziQo2OAG9mP9RDEi5lZYLtVUFgefz8dWb9fTMexdsx4RmqBEA=s16000
https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEg8Nloimfe6zD2aWpykEvsUGYBXjnvvoNHFknrBTbHk4jLnXnavPpjwy-Bnv3me1iSTexR2Ji07fk-9XbePE-WYPNpMZnYjtJy0kWdvza3ukbHFpLhu2u6moK1V9BqKDG5kgEkv2eh-wziQo2OAG9mP9RDEi5lZYLtVUFgefz8dWb9fTMexdsx4RmqBEA=s72-c
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/watanzania-940507-wapokea-chanjo-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/10/watanzania-940507-wapokea-chanjo-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy