CCM kuwatosa wala rushwa

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amezitaka kamati za siasa za wilaya na mkoa za chama hicho, kutowapitisha wag...

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amezitaka kamati za siasa za wilaya na mkoa za chama hicho, kutowapitisha wagombea wa chama hicho wanaotumia rushwa, kujenga makundi ndani ya chama hicho na kuanza kampeni kabla ya wakati.

Amesema hiyo ni siri pekee, itakayokifanya chama hicho kutenda haki na kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao wa madiwani, ubunge na urais.

Amesema kwa kutambua hilo, ndio maana Kamati Kuu ya Taifa ya chama hicho, imewachukulia hatua, wanachama wa chama hicho wanaotaka kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao lakini wakiwa wameanza kufanya kampeni mapema, na hivyo kukiuka kanuni na taratibu za chama hicho katika kuwapata wagombea.

Akiwahutubia mamia wa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Mpwapwa, Kinana alisema ni dhambi kwa mgombea uongozi wa CCM kutumia makundi, rushwa na kuanza kampeni mapema kama njia ya kumfanya kushawishi kupata uongozi na kusisitiza kuwa viongozi wanaotumia mbinu hizo kamwe hawawezi kuwaletea wananchi maendeleo.

Kinana yupo katika ziara ya kuutembelea mkoa wa Dodoma, aliyoikatisha kufuatia kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Mbunge wa Mbinga Magharibi na Kiongozi wa Kikundi cha Hamasa cha TOT, marehemu John Komba aliyefariki dunia Februari 28, mwaka huu na kuzikwa Machi 3, mkoani Ruvuma.

“Ukiona CCM imeshindwa katika uchaguzi wowote ule wala usihangaike kutafuta mchawi. Kushindwa kwa mgombea wa CCM mahala popote pale iwe ni Mpwapwa, Biharamulo au penginepo hutokana na sababu za ndani ya chama si nje, na sababu kubwa ni kutokana na kuwepo kwa makundi haramu ndani ya chama.

“Haiwezekani CCM ikashinda kama viongozi wanaohusika na uteuzi hawatendi haki, anakuwepo mgombea mzuri, anapendwa na watu, wanamheshimu, lakini yupo kiongozi fulani hamtaki, hii ndio chanzo cha migogoro yote inayotokea nchini. Viongozi wa CCM wanakula njama wanasema huyo tusimchague na badala yake wanakuja na jina la mgombea wa hovyo, hana sifa, mlanguzi au mlevi.

“Imefika mahala mtu anapewa uongozi ndani ya CCM kwa sababu ndani ya vikao vya uteuzi kuna ndugu zake, marafiki zake au watu wanaomhusu.Hili suala la uonevu hatutalivumilia mwaka huu, haiwezekani watu wa chini wanafanyiwa uonevu na viongoziwa juu wapo kimya. Ukiona kiongozi huyu anakaa kimya kwa masuala kama haya jua kunamambo mawili au anapendelea au kapewa rushwa,” alisema Kinana.

Kutokana na hilo, Kinana aliwataka wanaCCM kuwa wakali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu huku akisema viongozi wa chama hicho waliochaguliwa katika nafasi mbalimbali si wafalme bali ni viongozi waliochaguliwa kuwaongoza wanachama wa chama hicho.

Katika kile kinachoonesha kukerwa na tabia hiyo, Kinana aliutaka uongozi wa CCM Mkoa wa Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Adam Kimbisa, kuwasaka viongozi wote waliowaonea wagombea katika uchaguzi wa nafasi mbalimbali na kuwajadili katika vikao vya Kamati ya Siasa ya Wilaya na Mkoa na wakithibitika waondolewe haraka kwenye nafasi zao.

“Haiwezekani... mtu hafai, hana sifa, ukiulizwa nini? Kanipa pesa, au ni jamaa yangu mwishowe wanaCCM wanapata hasira wanakwenda kumpigia kura mgombea wa upinzani, hilo sasa mwisho wake umefika, tutapambana,” alisema Kinana akitolea mfano wa kiongozi wa upinzani katika mji wa Gairo, aliyechaguliwa kutokana na haki kukiukwa kwa mgombea wa CCM.

COMMENTS

BLOGGER
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: CCM kuwatosa wala rushwa
CCM kuwatosa wala rushwa
http://habarileo.co.tz/images/resized/images/kinana5_300_173.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/ccm-kuwatosa-wala-rushwa.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2015/03/ccm-kuwatosa-wala-rushwa.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy