UNGIZO jipya ndani ya Yanga, Khalid Aucho ameweka wazi kuwa sababu ya yeye kutosaini Simba ni kutofanya mazungumzo na timu hiyo moja kwa mo...
UNGIZO jipya ndani ya Yanga, Khalid Aucho ameweka wazi kuwa sababu ya yeye kutosaini Simba ni kutofanya mazungumzo na timu hiyo moja kwa moja.
Awali kabla ya kutangazwa rasmi jana kiungo huyo raia wa Uganda alikuwa anatajwa kuibukia Simba ambayo nayo pia ilikuwa inasaka saini yake.
Sababu kubwa ya yeye kukubali kutua Yanga ni raia wa Uganda akiwa amecheza timu zaidi ya 11 ikiwa ni pamoja na timu ya Gor Mahia ya Kenya pamoja na Tusker FC.
Kiungo huyo amesema:"Kweli Simba walikuwa wanahitaji saini yangu ila sikuzungumza nao moja kwa moja ni wakala wangu alizungumza nao, mimi nikapenda kusaini Yanga kwa kuwa ni timu kubwa,".
Ni dili la miaka miwili amepewa akiungana na Heritier Makambo, Fiston Mayele hawa wanatoka Congo, pamoja na kipa kutoka Mali, na mzawa Yusuph Athuman
Credit: SALEH JEMBE
Please subscribe to get all sports news instantly
COMMENTS