Dkt Gwajima Azindua Baraza La Taifa La Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali (Nacongo)
HomeHabari

Dkt Gwajima Azindua Baraza La Taifa La Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali (Nacongo)

 Na Mwandishi Wetu Dodoma Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amezindua Baraza jipya la Mash...

Watu Saba wafariki dunia kwa radi Katavi
MSD Kuwa Mkombozi Usafishaji Damu Kwa Wagonjwa Wa Figo
Wanafunzi Waliokuwa Mamekwama Katika Mji Wa Sumy – Ukraine Kuanza Kuondolewa

 Na Mwandishi Wetu Dodoma
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amezindua Baraza jipya la Mashirika Yasiyo ya kiserikali linalojumisha wajumbe kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na wawakilishi wa makundi mbalimbali.

Dkt.Gwajima amezindua Baraza hilo Juni10, 2021 jijini Dodoma mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi wa Baraza uliosimamiwa na Kamati ya mpito iliyoteuliwa na Waziri huyo June 07 2021.

Waziri Dkt. Gwajima amesema kuwa Baraza la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ni chombo cha uwakilishi na kiungo muhimu kati ya Mashirika na Serikali, hivyo uwepo wa Baraza hili utasaidia utekelezaji wa majukumu kwa mujibu wa Sheria.

“Niliamua kutekeleza Sheria kwa kuteua Kamati ya Mpito ya uchaguzi wa Baraza hili kwa sababu mimi kama msimamizi wa Sheria na Kanuni za Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nisingeweza kuvumilia vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na Kanuni hizo” alisema Waziri Dkt. Gwajima.

Pia Waziri Dkt. Gwajima ametoa wito kwa viongozi wa wajumbe wote wa Baraza kufanya kazi kwa weledi, uadilifu, na uzalendo wa hali ya juu kwa sekta ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na Taifa kwa ujumla ili kuhakikisha Sekta hiyo inafanya kazi kwa kuzingatia Sheria na Kanuni zilizopo.

“Uchaguzi umeshaisha sasa nendeni mkafanye kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ilioyopo ili kukidhi matarajio ya waliochagua na jamii ya Watanzania kwa ujumla” alisema Waziri Dkt. Gwajima

Aidha, Dkt .Gwajima ameliahidi Baraza hilo kutekeleza mapendekezo yao na kuwataka wajitoe kwa hali na mali kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha yale yaliyopendekezwa yanafanyiwa kazi kwa kasi na weledi.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto,Idara kuu ya Maendeleo ya jamii Dkt.John Jingu  amesema matarajio ya Wizara ni kuhakikisha NaCoNGO inafanya kazi kwa waledi ili kusaidiana na Serikali katika kutatua chanagamoto za wananchi katika kujiltea maendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Baraza la Mashirika yasiyo ya kiserikali Dkt. Lilian Badi amesema uongozi mpya utahakikisha panakuwa na uwajibikaji,na kuzingatia maadili katika utekelezaji wa majukumu wa Baraza hilo na kujenga mahusiano na taasisi zingine pamoja na kuzingatia Sheria zilizowekwa.

Akitoa maelezo ya uchaguzi Mwenyekiti wa Kamati ya mpito ya Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Wakili Flaviana Charles amesema mchakato wa uchaguzi ulifanywa kwa kuzingatia kanuni na demokrasia na imewezesha kupata viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya hadi taifa.

Aidha ameainisha mapendekezo kwa Baraza jipya kuwa ni pamoja na kuweka ratiba mapema ya chaguzi zijazo, uwiano wa uwakilishi,kuwa na data base, kuwajengea uwezo zaidi watumishi wa NaCoNGO na kupitia kanuni zilizopitwa na wakati  pamoja na kuwepo bajeti toshelezi ili kuweza kuendesha Baraza hilo kwa ufanisi


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Dkt Gwajima Azindua Baraza La Taifa La Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali (Nacongo)
Dkt Gwajima Azindua Baraza La Taifa La Mashirika Yasiyo Ya Kiserikali (Nacongo)
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRs5UmMrnNYZ05PYWAl9IkwBR29-V2ajMVFRsh-9AvXzC6fwACEp7cwk0p5-ZZ6UFpYAEVsxkXH6FUxbfx-OoobRGgfaonGtencw12UH8Jw4j3SH7eB96aVOa8RUxPRBFsLnMvIADNPv1e/s16000/1.webp
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjRs5UmMrnNYZ05PYWAl9IkwBR29-V2ajMVFRsh-9AvXzC6fwACEp7cwk0p5-ZZ6UFpYAEVsxkXH6FUxbfx-OoobRGgfaonGtencw12UH8Jw4j3SH7eB96aVOa8RUxPRBFsLnMvIADNPv1e/s72-c/1.webp
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/dkt-gwajima-azindua-baraza-la-taifa-la.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/07/dkt-gwajima-azindua-baraza-la-taifa-la.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy