HomeHabariTop Stories

Waziri wa usalama wa taifa Israel atishia kujiuzulu ikiwa watakubali kusitisha mapigano

Waziri wa Usalama wa Kitaifa wa mrengo mkali wa kulia wa Israel Itamar Ben-Gvir ametishia kujiondoa katika baraza la mawaziri la Waziri Mkuu...

Waziri wa Usalama wa Kitaifa wa mrengo mkali wa kulia wa Israel Itamar Ben-Gvir ametishia kujiondoa katika baraza la mawaziri la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu iwapo ataidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas baada ya zaidi ya siku 460 za vita huko Gaza.

Ben-Gvir alikashifu makubaliano hayo siku ya Alhamisi jioni na kusema chama chake cha Otzma Yehudit chenye uzalendo wa hali ya juu – pia kinachojulikana kama Jewish Power Party – kitajiondoa serikalini ikiwa usitishaji mapigano utakamilika.

“Ikiwa mkataba huu usio na uwajibikaji utaidhinishwa na kutekelezwa, chama cha Jewish Power Party hakitakuwa sehemu ya serikali na kitauacha,” alisema.

Ben-Gvir pia alisema misaada ya kibinadamu na mafuta, umeme na maji lazima “ikomeshwe kabisa” kuingia katika eneo lenye vita la Palestina ili kulazimisha kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas.

“Hapo ndipo Hamas itawaachilia mateka wetu bila kuhatarisha usalama wa Israeli,” alisema.

Vile vile amemtaka Waziri mwenzake wa Fedha wa mrengo wa kulia wa Israel Bezalel Smotrich, Mkuu wa Chama cha Kidini cha Kizayuni na mkosoaji mwingine wa usitishaji vita, ajiondoe kwenye baraza la mawaziri iwapo usitishaji huo wa mapigano utaidhinishwa.

The post Waziri wa usalama wa taifa Israel atishia kujiuzulu ikiwa watakubali kusitisha mapigano first appeared on Millard Ayo.



from Millard Ayo https://ift.tt/CgA3uXJ
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waziri wa usalama wa taifa Israel atishia kujiuzulu ikiwa watakubali kusitisha mapigano
Waziri wa usalama wa taifa Israel atishia kujiuzulu ikiwa watakubali kusitisha mapigano
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/waziri-wa-usalama-wa-taifa-israel.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2025/01/waziri-wa-usalama-wa-taifa-israel.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy