Tanzania, Saudi Arabia Zaahidi Ushirikiano Katika Elimu
HomeHabari

Tanzania, Saudi Arabia Zaahidi Ushirikiano Katika Elimu

Na Mwandishi Wetu, Dar   Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Saudi Arabia zimeahidi kuendelea kushirikiana na kuku...

Habari kubwa Magazetini Kenya leo November 24, 2024
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo November 24, 2024
Alikiba akishirikia na Asas waandaa tamasha la ASAS FIT & FUN KIDS FEST


Na Mwandishi Wetu, Dar
 
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Saudi Arabia zimeahidi kuendelea kushirikiana na kukuza sekta elimu kwa manufaa ya mataifa yote mawili.
 
Ahadi hiyo imetolewa na Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Abdullah Ali Alsheryan alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb)  katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
 
Balozi Alsheryan amemhakikishia Balozi Mbarouk kuwa Saudi Arabia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuendeleza sekta ya elimu ambapo kwa mwaka 2022 Saudi Arabia imetoa fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 80 wa kada mbalimbali.
 
“Serikali yetu kwa kutambua mchango wa elimu, imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 80 wa kitanzania, hivyo ni rai yangu kwa watanzania kuchangamkia fursa hizo pindi zitakapotangazwa,” alisema Balozi Alsheryan
 
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Saudi Arabia katika kukuza na kuendeleza ushirikiano imara baina ya mataifa hayo uliodumu kwa muda mrefu.
 
“Uhusiano wa Tanzania na Saudi Arabia umezidi kuimarika, pia tumefurahishwa na fursa za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wetu na tunaahidi kutumia fursa hiyo kwa maendeleo ya taifa letu” amesema Balozi Mbarouk.
 
Ushirikiano wa Tanzania na Saudia Arabia ni wa muda mrefu ambapo mataifa hayo yamekuwa yakishirikiana katika Nyanja za nishati na gesi, madini, utalii na kilimo, afya, elimu na kiutamaduni.
 



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania, Saudi Arabia Zaahidi Ushirikiano Katika Elimu
Tanzania, Saudi Arabia Zaahidi Ushirikiano Katika Elimu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg489Wv1tpRwTt5rdEaQKy1EXhoGvXXNSNxOYTIT89nwO4MW9-kM9NjMtImAnz6x8IESaQcAGW7wJZ40-v71u2X3vPYm6vSbHcnNZBlqPfQm7OPORYo6lboKQuXTlaG2XIpeI387FYGLUCt_ndM7UyhBVCwNy5aIdejaVXQoa5wXf4LiwlqUu6pERhbSw/s16000/1.png
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg489Wv1tpRwTt5rdEaQKy1EXhoGvXXNSNxOYTIT89nwO4MW9-kM9NjMtImAnz6x8IESaQcAGW7wJZ40-v71u2X3vPYm6vSbHcnNZBlqPfQm7OPORYo6lboKQuXTlaG2XIpeI387FYGLUCt_ndM7UyhBVCwNy5aIdejaVXQoa5wXf4LiwlqUu6pERhbSw/s72-c/1.png
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/tanzania-saudi-arabia-zaahidi.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/06/tanzania-saudi-arabia-zaahidi.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy