Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria Watakiwa Kuripoti Makambini
HomeHabari

Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria Watakiwa Kuripoti Makambini

Na Mwandishi wetu- Dodoma Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali  Rajabu Mabele amewataka  vijana wote waliochaguliwa k...

Wabunge Waitwa Dodoma Kwa Ajili Ya Shughuli Za Kamati Za Kudumu Za Bunge
Makamu Wa Rais Ashiriki Jukwaa La Uchumi Duniani
Wizara Ya Afya Na Shirika La Afya Duniani Zasaini Mpango Wa Utekelezaji Wa Afua Za Afya Wenye Thamani Ya Shilingi Bilioni 49.2


Na Mwandishi wetu- Dodoma

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali  Rajabu Mabele amewataka  vijana wote waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa  Sheria kwa mwaka 2021 ambao hawajaripoti na wale waliochanguliwa kwa awamu ya pili kuhakikisha wanaripoti kwa wakati katika makambi waliyopangiwa kufikia June 17,  2021 ili waweze kuanza mafunzo hayo kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Hassan Mabena    Juni 10, 2021, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu  ya JKT Chamwino mkoani Dodoma.

“Mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria mwaka 2021 yataendeshwa kwa muda wa miezi mitatu tu, vijana hao walioitwa kupitia orodha ya pili na baadhi ya wale  wa awamu ya kwanza ambao hawajaripoti hadi sasa wanatakiwa kuripoti makambi ya JKT  waliyopangiwa mara moja”, alisisitiza  Kanali  Mabena

Akifafanua, Kanali Mabena amesema kuwa kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (Physical disabilities)  wanatakiwa kuripoti katika kambi ya Ruvu   JKT  iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuwahudumia.

Orodha kamili ya nyongeza ya majina ya vijana walioitwa , Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo yaliyopo pamoja na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz.

Aidha, Mkuu wa JKT Brigedia Jenerali   Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote walioitwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa.





Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria Watakiwa Kuripoti Makambini
Waliochaguliwa JKT Mujibu wa Sheria Watakiwa Kuripoti Makambini
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdXXcj0tLq-ietuS4OSoBc3XbPP6TjuHFzWixHn0v81JV5-XpxRj9DqNgYZLTdkLGpKIUtQzkRGhL_YgPO3EAaSr2Z1Dkz7D_HVj9D3ILQB-R6_NPsFg2lv0zFwAmATzCHj1ammDD2qAV6/s16000/CB3A9869.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjdXXcj0tLq-ietuS4OSoBc3XbPP6TjuHFzWixHn0v81JV5-XpxRj9DqNgYZLTdkLGpKIUtQzkRGhL_YgPO3EAaSr2Z1Dkz7D_HVj9D3ILQB-R6_NPsFg2lv0zFwAmATzCHj1ammDD2qAV6/s72-c/CB3A9869.JPG
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/waliochaguliwa-jkt-mujibu-wa-sheria.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/06/waliochaguliwa-jkt-mujibu-wa-sheria.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy