Mwanza kunufaika na Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu
HomeHabari

Mwanza kunufaika na Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu

Na Asteria Muhozya, Dodoma Kukamilika kwa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Madini ya Dhahabu kwa kiwango kikubwa barani Afrika cha Mwanza...

MAMIA YA WAKAZI WA KIGAMBONI WANAOTUMIA USAFIRI WA MV KIGAMBONI WAMEKWAMA KWA ZAIDI YA SAA MBILI
Serikali kunusuru machinga nchini
Magari ya utalii Tanzania yakataliwa kuingia JKIA


Na Asteria Muhozya, Dodoma
Kukamilika kwa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Madini ya Dhahabu kwa kiwango kikubwa barani Afrika cha Mwanza Precious Metals Refinery Ltd kinatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi Mkoani humo na Taifa, hususan kupitia biashara ya madini.

Aidha, Kiwanda hicho kinachotajwa kuwa na teknolojia ya kisasa ya kusafisha dhahabu mpaka 999.9 purity kinapelekea dhahabu kutoka Tanzania kuwa na ubora wa kimataifa wa kununuliwa na Benki Kuu duniani kwa ajli ya kuhifadhiwa.

Hayo yamebainishwa  Machi 10, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse wakati akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi wa kiwanda hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, jijini Dodoma.

Dkt. Mwasse ameongeza kuwa, kiwanda hicho kimewekewa uwezekano wa kuongeza uzalishaji wa hadi kilo 960 kwa siku tofauti na kilo 480 kwa siku ambazo zimepangwa kusafishwa mara baada ya kuanza kazi mwishoni mwa mwezi Machi, 2021.

Pia, Dkt. Venance amesema kuwa, ujenzi wa kiwanda hicho ambacho ni kikubwa kwa usafishaji dhahabu, ikilinganishwa na mitambo ya nchi za Afrika ya Kusini na Sudan ni matokeo ya Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 ambayo yalichangiwa na kutungwa kwa Sheria ya Natural Wealth and Resources (Permanent sovereghty ya mwaka 2017, ambayo iliweka msisitizo kuhusuiana na rasilimali za nchi na matakwa ya nchi kufaidika na madini yanayochimbwa nchini kwa kuyaongezea thamani kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.

Akizugumzia vyanzo vya malighafi katika kiwanda hicho amesema, vitatoka kwa wachimbaji wadogo kupitia mradi wa kusaidia wachimbaji wadogo (ASM Support project), wachimbaji wakubwa wenye migodi hapa nchini, dhahabu kutoka nchi jirani na dhahabu kutoka kwa madalali.

Akifafanua kuhusu faida za ujenzi wa kiwanda hicho amesema kuwa ni pamoja na kuongeza mapato kwa nchi kupitia mrabaha na ada za ukaguzi, kuongeza mapato ya Halmashauri kilipo kiwanda hicho kupitia ushuru wa huduma, kuongeza ajira kwa taifa ambapo mradi unatarajia kuajiri watumishi 120 wengi wakiwa watanzania na wachache kutoka nje ya nchi ikihusisha ajira za wakandarasi, wazalishaji wa dhahabu, wazabuni, watoa huduma na wasafirishaji.

Vilevile, amezitaja faida nyingine za ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni pamoja na kuwezesh Benki Kuu kuanza kununua dhdhabu kwa mujibu wa sheria za nchi, serikali kuanza kukusanya mrabaha kwa kuchukua dhahabu badala ya fedha, dhahabu inayozalishwa Tanzania kuanza kutambulika na kuwa na nembo yake maluum, kuwa na kituo cha kuuza tofari za dhdhabu kutoka kwa wazalishajimbalimbali wa dhahabu ndani na nje ya nchi na huduma wa jamii inayozunguka mradi huo.

Mradi wa Mwanza Precious Metals Refinery ni Ubia kati ya STAMICO, kampuni ya Rozelia General Trading LLC ya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na Kampui ya ACME Consultant Engineers PTE Ltd ya Singapore. STAMICO inamiliki asilimia 25 na wabia asilimia 75.

Aidha, kulingana na taarifa ya Dkt. Mwasse kwa Kamati, amesema hisa za STAMICO zitakuwa zikiongezeka kwa asilimia 5 kwa kipindi cha miaka 15 na hivyo kuifanya STAMICO kumiliki asilimia 51 na wabia asilimia 49.

Vilevile Dkt. Mwasse amesema STAMICO itakuwa inapata asilimia 2.5 ya mauzo ghafi kama ada ya huduma za usimamizi .


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Mwanza kunufaika na Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu
Mwanza kunufaika na Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdDa1RSG0-ujeGEWTQKqYPNgssSL6gjV_-cxdEmARFRpgJ9NY4E-2Dmbuoo8Qm8YA6xRepxxj90GOHAxWnlAB31aS3pq-B7qYP7mE45s5itchcpIbl7yU24M5UNlxuVd8Oq0jOWB1AKPp8/s16000/1.jpeg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgdDa1RSG0-ujeGEWTQKqYPNgssSL6gjV_-cxdEmARFRpgJ9NY4E-2Dmbuoo8Qm8YA6xRepxxj90GOHAxWnlAB31aS3pq-B7qYP7mE45s5itchcpIbl7yU24M5UNlxuVd8Oq0jOWB1AKPp8/s72-c/1.jpeg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/mwanza-kunufaika-na-kiwanda-cha.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/03/mwanza-kunufaika-na-kiwanda-cha.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy