Mamia ya wakazi wa Kigamboni ambao wanatumia usafiri wa MV Kigamboni wamekwama kwa zaidi ya saa mbili h...
Mamia
ya wakazi wa Kigamboni ambao wanatumia usafiri wa MV Kigamboni
wamekwama kwa zaidi ya saa mbili huku wengine wakilazimika kutumia
viboti vidogo kwa ajili ya kuvuka upande wa pili ili kuwahi katika
shughuli zao kufuatia kutokuwepo kwa kivuko hicho na hivyo kutumika kwa
kivuko kimoja tuu.
Wakizunguza
kivukoni hapo baadhi ya waathirika wa tukio hilo wamesema wamelazikia
kugombea kivuko kimoja kilichokuwa kikifanya kazi huku wengine hasa
wanafunzi wanaosoma chuo cha usimamizi wa fedha IFM ambao wengi wao
wanaishi Kigamboni kujikuta wanachelewa kwenye mitihani.
Kutokana
na hali hiyo ya kivuko kujirudia rudia kuharika baadhi ya watumiaji wa
kivuko hicho wameshauri ni bora huduma za vivuko hizo zikabinafishshwa
ili kupata mwekezaji atakayeweza kuviendesha vivuko hivyo kwa uhakika
kabla madhara zaidi hayajatokea.
Tuliutafuta
uongozi wa wakala wa ufundi na umeme Temesa kuzungumzia hali hiyo
ambapo afisa mtendaji mkuu Bi Marcellin Magesa amesema kivuko hicho
kilikuwa katika matengenezo ya kawaida na kilipokuwa kilifanyiwa
matengenezo kilipoteza mwelekeo injini zikazima baada ya kuingia
takataka.
COMMENTS