Upatikanaji umeme wapunguza matumizi ya mafuta ya Taa nchini
HomeHabari

Upatikanaji umeme wapunguza matumizi ya mafuta ya Taa nchini

 Na Zuena Msuya Dodoma, Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema usambazwaji na upatikanaji wa umeme vijijini umepunguza kwa...

Mfumo Wa Mashtaka Ufanane Nchi Nzima – Mpanju
Tanzania kupeleka timu 4 kimataifa Msimu Ujao wa 2021/2022
VIDEO: Lady Jaydee – I Love MySelf


 Na Zuena Msuya Dodoma,
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani amesema usambazwaji na upatikanaji wa umeme vijijini umepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya mafuta ya taa nchini.

Dkt.  Kalemani alisema hayo tarehe 11 Februari, 2021 wakati wa semina iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, iliyokuwa na lengo la kuieleza kamati hiyo majukumu ya Wizara pamoja na Taasisi zilizo chini yake.

“Kwa sasa matumizi ya mafuta ya taa yamepungua hadi kufikia takribani lita 110,000 kwa siku tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, ambapo lita zaidi ya 140,000 zilikuwa zikitumika kwa siku na hii inatokana na shughuli nyingi za kijamii vijijini kutumia umeme.” Alisema Dkt.Kalemani

Aliongeza kuwa, mafuta ya taa yalikuwa yakitumika kama chanzo cha mwanga vijijini, ambapo sasa asilimia kubwa ya wakazi wa vijijini wanatumia umeme kujipatia mwanga.

“Sasa hivi matumizi ya mafuta ya taa yamepungua sana na yanaendelea kupungua siku hadi siku, kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya umeme, hii inatokana na juhudi zenu ninyi wabunge pamoja na Serikali kuhakikisha kuwa umeme unasambaa vijijini.” Alisema Dkt. Kalemani

Kuhusu kuongezeka kwa matumizi ya Mafuta ndege, Dkt. Kalemani alisema kuwa kwa sasa matumizi ya mafuta hayo yameongezeka kutokana na kuwepo kwa safari nyingi za ndege zinazomilikiwa na serikali.

Alisema kuwa, kwa sasa Tanzania inamiliki ndege nyingi ambazo hufanya safari zake ndani na nje ya nchi, hivyo kufanya mafuta hayo kutumika kwa wingi.

Alifafanua kuwa, matumizi ya mafuta ya ndege yamepanda hadi kufikia lita Laki Sita kwa siku tofauti na huko nyuma matumizi yalikuwa chini ya Lita Laki Tatu kwa siku.

Katika hatua nyingine, alisema kuwa, Serikali inaendelea na mpango wa kuanzisha vituo vidogo vya mafuta katika maeneo ya vijijini ili kusogeza karibu huduma ya mafuta ya Petroli, Dizeli na Taa.

Alisema kuwa, mpango huo utaondoa adha kwa wananchi kutembea umbali mrefu kufuata bidhaa hiyo, na pia kuondoa hatari inayoweza kuwakumba watu wanaohifadhi bidhaa hiyo ndani ya nyumba zao.

Taasisi zilizo chini ya Wizara, zilizoshiriki Semina hiyo ni Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Kampuni ya Uendelezaji JotoArdhi Tanzania( TGDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA), Mamlala ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).


Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Upatikanaji umeme wapunguza matumizi ya mafuta ya Taa nchini
Upatikanaji umeme wapunguza matumizi ya mafuta ya Taa nchini
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzRh__pWPznbI2px1BHr1osb7xou7ALgnSqFCekxMEEf8tRt9Im0NzIJ6ftRDuQYcJvuLsy_fPYuQhMGIkYqE5gkQ7sibPOV0A7nx7Vzk2VWfIF2ZaFVsn32e0QEoUWjRII6QIfw2ZLSXt/s16000/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzRh__pWPznbI2px1BHr1osb7xou7ALgnSqFCekxMEEf8tRt9Im0NzIJ6ftRDuQYcJvuLsy_fPYuQhMGIkYqE5gkQ7sibPOV0A7nx7Vzk2VWfIF2ZaFVsn32e0QEoUWjRII6QIfw2ZLSXt/s72-c/1.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/upatikanaji-umeme-wapunguza-matumizi-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2021/02/upatikanaji-umeme-wapunguza-matumizi-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy