Tanzania Imefikia Asilimia 37 Ya Uchanjaji Chanjo Ya Uviko-19
HomeHabari

Tanzania Imefikia Asilimia 37 Ya Uchanjaji Chanjo Ya Uviko-19

Na.Catherine Sungura,Tanga Hadi kufikia tarehe 18 Julai, 2022 jumla ya wananchi milioni 11.5 sawa na asilimia 37 ya watu wenye umri wa m...


Na.Catherine Sungura,Tanga

Hadi kufikia tarehe 18 Julai, 2022 jumla ya wananchi milioni 11.5 sawa na asilimia 37 ya watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wamepata chanjo kamili ya UVIKO-19 hapa nchini.

Hayo yamebainishwa leo Tarehe 20/7/2022 na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakati wa kikao cha Viongozi wa dini wa Mkoa wa Tanga ikiwa ni mkakati wa uhamasishaji wa kuongeza kasi ya kuchanja nchini.

“Tumeshachanja watu milioni 11.5 wamepata kinga kamili kati ya watu milioni 30.7 ambao tumewalenga, sasa hivi imethibitika pasi na shaka kwamba chanjo ndio njia pekee ya uhakika inayoweza kupunguza makali ya UVIKO-19 na ili tuweze kutengeneza kinga ya jamii, dunia imejiwekea malengo angalau tuweze kuchanja asilimia 70 ya watu wote duniani” Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amebainisha kwamba   idadi hiyo imefikiwa kutokana na kampeni iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan mwaka 2021 ikiwemo huduma tembezi, kusogeza vituo vya kuchanja karibu na  maeneo ya watu ambapo vituo vya kutolea chanjo vilikua  550 mwaka 2021 na kufikia vituo 7000 mwaka 2022.

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inatambua na itaendelea kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi za dini hapa nchini katika mapambano dhidi ya magonjwa ikiwemo ugonjwa wa UVIKO-19 hivyo kikao hicho kitaleta mbinu mbalimbali za kuwafikishia wananchi.

“Tunaamani kabisa ninyi viongozi wa dini mnajihusisha kwenye mambo ya jamii mna mambo makubwa ya kutufundisha na mtatupatia mbinu na mikakati mbalimbali za kwenda kuwahamasisha wananchi, ninyi tangu ugonjwa huu kuingia nchini mmekua mnatusaidia  kufikisha elimu kwa jamii kujikinga na ugonjwa huu” amesema Waziri Ummy

Kuhusu hali ya uchanjaji kwa Mkoa wa Tanga Waziri Ummy amesema Mkoa wa Tanga ipo asilimia 22 kati ya asilimia 37 ya Kitaifa na  Wilaya ya Muheza  wamechanja asilimia 69 na kufuatiwa na Pangani asilimia 40, Korogwe mji 38, handeni mji 35 na Tanga jiji asilimia 26.



Credit: MPEKUZI

Thanks for your time please share with your friends
Name

Afya,4,Ajira,2657,Audio,26,Biashara,2,Burudani,43,Economics,1,ELIMU,26,Gossip,38,Habari,3618,History,2,Kimataifa,202,kisiasa,13,Kiswahili,6,Kitaifa,147,Magazeti,44,Matokeo,3,Matukio,89,Michezo,2829,Muziki,62,Nairobi aiport,1,Ripoti,4,Tools,1,Top Stories,757,Video,47,Vituko,15,
ltr
item
Antagon Blog: Tanzania Imefikia Asilimia 37 Ya Uchanjaji Chanjo Ya Uviko-19
Tanzania Imefikia Asilimia 37 Ya Uchanjaji Chanjo Ya Uviko-19
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTbCxuJAIfAbwfQOrxJr8hk57DS6mRTzlvtm3k_J5Aqpdku6Z-lu9K1mzkr5hhsOnOZM7H_P8Gv53oVlCClF5DnXQA3WW3dEtBYvYXC85Y-cLnUBlKxSDd8bOJi4-dl8vaXhaktTRu62ukfMujbxn1ukjkZxiRENSDQY2PKsLb9c6ndtjnOpXt8Ryh1g/s16000/InShot_20220720_175630029.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgTbCxuJAIfAbwfQOrxJr8hk57DS6mRTzlvtm3k_J5Aqpdku6Z-lu9K1mzkr5hhsOnOZM7H_P8Gv53oVlCClF5DnXQA3WW3dEtBYvYXC85Y-cLnUBlKxSDd8bOJi4-dl8vaXhaktTRu62ukfMujbxn1ukjkZxiRENSDQY2PKsLb9c6ndtjnOpXt8Ryh1g/s72-c/InShot_20220720_175630029.jpg
Antagon Blog
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/tanzania-imefikia-asilimia-37-ya.html
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/
https://antagonf.blogspot.com/2022/07/tanzania-imefikia-asilimia-37-ya.html
true
8268252095325502418
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy